HIZI NI KELELE ZA KIMASA KWA UKOSEFU WA MAENDELEO NCHINI!!


Neno ama msamiati fadhila lina maana pana kama ukilingalia kwenye kamusi, lakini kwa jinsi linavyotumika kwa watu wengi kwa wakati huu na hasa linapokuja suala la rushwa ni kwamba inakuwa ni msaada ,shukurani ama asante !Hali hii ni kwa wahusika wote ambao wamehongana ama waliopeana huduma kwa kutoa ama kupokea rushwa.

Kwa wakati huu rushwa imetanda karibu kila sekta , iwe ni katikab vyombo vya habari , hospitali , kwenye huduma za usafiri , bandarini ,polisi, PCCB, Mamlaka ya Leseni, ama sehemu yoyote ile.Hivyo, neno fadhila linatamba kisawa sawa katika anga za rushwa!Ingawa watoaji na wapokeaji bado wana maneno yao mengine mengi ukiachiliambali neno fadhila.

Tusibishane! Ni kweli rushwa inachukua nafasi kubwa kwa wakati huu katika maisha yetu ya kila siku Watanzania, na hii inatokana na kwamba Watanzania wengi hatuna ustarabu wa kusubiri , kwa mfano utakuta mtu anakwenda hospitali , huko akikuta kuna foleni ya kuingia kwa daktari atataka kumhonga nesi eti amuingize haraka kwa daktari ili ahudumiwe yeye kwanza na kuwaacha wananchi wengine aliowakuta kwenye foleni!Kisayeye anataka "favour ".Huo ni upuuzi na bado kuna upuuzi mwingi kama huu karibu kwenye kila huduma hapa Bongo.Hebu siku moja jaribu ama jifanye unataka kukata tiketi ya ndege kwenda ulaya !Utajionea vioja na mambo mengi kwa hao maajenti wa hizo tiketi.

Lakini tutaendelea kuishi hivi hadi lini? Yaani mambo hayaendi bila kutoa kitu kidogo? Hapana budi . Tutambue kwamba rushwa inadidimiza uchumi na maendelea kwa wakati mmoja.Wananchi tukisema hapana kwa rushwa kweli itakuwa hapana . Tusiposema hapana kelele kama zangu za ukosefu wa maendeleo zitaendelea kupigwa na mimi na wengine leo , kesho hata siku nyingine.Ni mimi Kimasa kutoka http://www.kingkif.blospot.com/.pia unawezakunipata kwa kingkif07@gmail.com ama 0714-077040

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment