Fataki ni Nani? hebu mcheki hapa akivinjari na Mwanafunzi!!

Fataki ni husika ya kufikirika aliyovikwa mwanaume mtu mzima ambaye anarubuni watoto wa kike pamoja na wanawake wengine ili kufanya nae ngono.
Fataki ni baba mtu mzima ambaye anatumia uwezo wake wa kiuchumi/kifedha kuwarubuni watu wa jinsia ya kike kutimiza lengo lake, kutokana na sifa yake hii anafikia hatua ya kubandikwa majina mengine kama ATM.
Shirika lisilo la kiserikali la The Strategic Radio Communication for Development (STRADCOM), lenye makazi yake Msasani, Dar es Salaam ndio hasa watunzi wa mradi huu wa Fataki. Wakufunzi Chip na Dan Heath, ambao pia ni waandishi wa kitabu maarufu cha “Made to Stick, waliendesha warsha ya wiki moja ya kuunda husika hii. Warsha ilifanyika August 2007 katika ofisi za STRADCOM.
Kwa kuanzia STARDCOM walitoa wazo ili lijadiliwe na wasanii/waigizaji na watayarishaji chini ya uongozi wa Chip na Dan, na matokeo ya majadiliano haya yakachukuliwa na kutengenezwa kwa ufasaha zaidi katika uumbaji wa husika ya Fataki.
Kampeni hii imekuwa ikisambazwa kwa kutumia matangazo ya radio, televisheni, mabango barabarani, pamoja na viponzo kwenye majarida.
http://www.wahapahapa.com

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment