Arsenal kuikabili Porto bila vigogo!

Arsenal imesafiri hadi Ureno kuikabili Porto bila ya wachezaji kadha wa kikosi cha kwanza katika hekaheka za Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.
Andrey Arshavin ana maumivu ya paja, matatizo yanayomkabili pia Eduardo aliyeshindwa kusafiri, wakati William Gallas akiwa anasumbuliwa na matatizo ya mgongo nae hajakwenda Ureno.
Mlinda mlango Manuel Almunia ana matatizo ya kidole na Alex Song anasumbuliwa na goti, nao hawatacheza. Wachezaji hao wanaungana na washambuliaji Robin van Persie na Carlos Vela ambao nao ni majeruhi.
Porto huenda wakamkosa mchezaji wao mahiri Ruben Micael kutokana kuumwa bega. http://www.bbcswahili.com/

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment