Wanamitindo hapa nchini wamanzisha chama chao kinachoitwa Tanzania Model Group (TMG) kitakachoshughulikia haki zao za msingi na kusimamia kazi zao zote zitakazofanywa na wanamitindo hao tofauti na hapo awali ambapo walikuwa wakifanya kazi mbalimbali kupitia mawakala (Agencys) mbalimbali zilizopo hapa nchini.
kuanzishwa kwa umoja huo kunadhihirisha kwamba wanamitindo hao wamechoka kudhulumiwa maslahi yao hivyo wameamua kuyasimamia wenyewe kwani wao ndiyo wanaofanya kazi hiyo ya uanamitindo hivyo wanawajibika kuyasimamia na kuhakikisha wanalinda haki zao za msingi.
Chama hicho kimesajiriwa na Baraza la Sanaa Tanzania BASATA na kinaanza kazi mara moja. Akizungumza na waandishi wa habari Katibu mkuu wa chama hicho Angel Yustace amesema madhumuni ya kuanzishwa kwa Tanzania Model Group ni kusimamia na kuendeleza sanaa ya mitindo kulingana na taratibu za kisheria, kuwezesha wanamitindo kutambuliwa, kuheshimika, kuthaminiwa na kinua fani ya mitindo kwa hadhi ya kitaifa na kimataifa, kushiriki na kutayarisha maonyesho mablimbali ya mavazi na wanamitindo kushiriki kwenye video mbalimbali pamoja na filamu.
akizungumzia upatikanaji wa wanachama na aina yake amesema kamati ya utendaji ndiyo inayopendekeza watu watakaopewa uanachama ikiwa ni pamoja na wanamitindo wa zamani kutokana na nafasi zao ndani ya jamii na mchango wao katika sanaa ya mitindo
Amesema sifa za uanachama ni kwa mtu yeyote ambaye ana akili timamu na atakayekubaliana na masharti ya kikundi, awe raia wa Tanzania, awe na umri usiopungua miaka 18 au usiozidi miaka 35, awe na vigezo vya kuwa mwanamitindo na mwisho awe mwenye kujiheshimu mwaminifu kwa wanakikundi na viongozi na kwa jamii kwa ujumla
0 comments:
Post a Comment