Na Veronica Kazimoto – MAELEZO
Taarifa kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa zinasema chama hicho kimefutiwa usajili kwa kutotekeleza sheria namba 5 ya vyama vya siasa ya mwaka 1992 inayosema kuwa ni lazima chama kiwe na wanachama 200 au zaidi.
Kwa mujibu wa sheria hiyo, chama cha Peoples Democratic Movement hakikuweza kufikisha idadi hiyo ya wanachama, hivyo msajili wa vyama vya siasa ameamua kukifutia usajili wake wa muda.
Wakati huo huo chama cha Democratic National Congress (DNC) kimekataliwa na msajili wa vya siasa kuongezewa muda wa usajili kwa mara ya tatu na hivyo kufutiwa usajili wake wa muda.
Taarifa ya msajili wa vyama vya sisa imebainisha kuwa, sheria ya vyama vya siasa namba 5 ya mwaka 1992 kifungu cha 8 (4) inaeleza kwamba usajili wa muda wa chama chochote utakoma kuendelea baada ya kuisha muda wa siku 180
Kwa mujibu wa sheria hiyo, chama cha DNC kimepitiliza muda huo na tayali kilishawahi kuongezewa muda mara mbili. Chama hicho kilisajiliwa mwaka 2008 na mpaka sasa takribani mwaka mzima umekwishapita.
0 comments:
Post a Comment