Serikali kuanzisha mtaala wa magonjwa ya Kansa Nchini!!

Prof. David Mwakyusa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii.
Benjamin Sawe
Maelezo Dar es Salaam
Kutokana na upungufu na madaktari Bingwa wa Ugonjwa wa Kansa katika Taasisi ya Kansa Ocean Road,Kaimu Mkurugenzi wa taasisi hiyo amesema Serikali ina mpango wa kuanzisha mtaala wa magonjwa ya kansa katika chuo kikuu kishiriki cha Muhimbili.
Dokta Mahunda alisema pia wameshapeleka Daktari mmoja Nchini Afrika Kusini kwa ajili ya mafunzo hayo ikiwa ni hatua kupunguza tatizo hilo linaloonekana kuielemea hospitali hiyo.
Daktari Mahunda alisema tatizo la upungufu wa madaktari bingwa wa kutibu kansa katika taasisi hiyo linatokana na vijana wengi kukimbia fani hiyo kwa kisingizio cha ugumu wake.
“Tumekuwa tukiwapa mafunzo ya kitaalamu zaidi vijana wengi hapahapa kwenye taasisi lakini cha kushangaza wengi wao wamekuwa wakikimbia hivyo kupelekea kuwa na upungufu mkubwa wa madaktari bingwa.
Aidha Dokta Mahunda alisema tayari baadhi ya madaktari wameshaongezewa mikataba ya kuendelea kufanyakazi katika taasisi hiyo ikiwa ni hatua kuendelea kuwapatia huduma wananchi.
Pia Dokta Mahunda alisema tatizo la madaktari bingwa sio la taasisi ya Ocean Road pekee bali linaikabili sekta nzima ya afya nchini.
“Tatizo la madaktari bingwa si la Taasisi ya Ocean Road pekee bali ni la sekta nzima ya afya nchini na Serikali ina mkakati mkubwa wa kukabiliana na tatizo hilo.
Hivi karibuni katika semina ya vyombo vya habari iliyohusu habari za kansa iliripotiwa kuwa katika taasisi ya magonjwa ya Kansa Ocean Road kuna madaktari bingwa watano ambao wanakaribia kustaafu hivyo kupelekea upungufu wa wataalamu hao hospitalini hapo.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment