Serikali ya Algeria inasema ina mipango ya kuwasafirisha kwa ndege mamia ya mashabiki Angola kwa mechi ya nusu fainali dhidi ya Misri.
Maelfu ya raia wa Algeria walisafirishwa kwa ndege hadi Sudan mwezi Novemba mwaka jana walipowafunga Misri 1-0 katika mechi ya kuania kufuzu kwa kombe la dunia.
Waziri wa mambo ya nje wa Algeria Mourad Medcli anasema mipango tayari imeshafanywa.
Hali ya wasiwasi inatarajiwa katika mechi ya nusu fainali siku ya Alhamisi huko Benguela kufwatia matatizo yaliyojitokeza wakati timu hizo zilipokutana mwezi Novemba.
Basi lilokuwa limewabeba wachezaji wa Algeria lilishambuliwa na mashabiki wa Misri mjini Cairo kabla ya mechi yao ya kuania kufuzu ambapo Misri ilipata ushindi wa magoli 2-0 kulazimisha mechi moja ya kuamua nani ataenda Afrika Kusini kwa kombe la dunia kuchezwa nchini Sudan.

0 comments:
Post a Comment