wachezaji wa Tusker ya Kenya wakiwa katika hekaheka katika moja ya michezo ambayo wameshiriki
Timu ya Yanga ya jijini Dar es salaam leo imefanikiwa kuifurumusha timu ya Tusker kutoka kenya baada ya kuifunga magoli 3-1 kwenye uwanja wa Uhuru katika michuano ya Kombe la Tusker inayoendelea hapa nchini.
Yanga ilijipatia goli lao la kuongoza katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo kupitia mshambuliaji wake hatari Mrisho Ngassa aliyefunga katika dakika ya 31 ya mchezo huo jambo ambalo liliifanya timu hiyo kuendelea kuwa na uchu wa kujipatia magoli mengine hata hivyo wachezaji timu Tusker walijitahidi kuzuaia hatari mpaka kipindi cha kwanza kilipomalizika.
Baada ya mapumziko timu ziliingia uwanjani katika ngwe ya lala Salama huku Yanga ilishambulia vilivyo lango la Tusker na mashambulizi hayo yalizaa matinda baada ya Jerry tegete wa Yanga kujipatia goli la pili katika dakika ya 47 huku mashabulizi yakongezeka kila muda uliposogea mwishoni.
Jeryy Tegete wa timu ya Yanga alikandamiza msumari wa mwisho kwa kuifungia goli la tatu timu yake kattika dakika ya 65 hivyo kuifanya Yanga kuibuka na ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya timu ya Tusker kutoka kenya ambayo ilipata goli la kufutia machozi kupitia mchezaji wake Collins Okoth katika dakika ya 67, hata hivyo matokeo hayo hayana athari kwa timu zote mbili kwani tayari zimeshatinga nusu fainali ya michuano hiyo ambapo Simba sasa itakutana na watani wao wa jadi timu ya Yanga huku timu ya Tusker ikikutana na ndugu zao Sofapaka kutoka Kenya pia.
0 comments:
Post a Comment