Benjamin Sawe
Maelezo Dar es Salaam
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Profesa Herman Mwansoko amewaasa madaktari wanawake wa tiba ya viungo kujiendeleza kielimu kwani wataalamu hao ni pungufu.
Profesa Mwansoko aliyasema hayo jana katika ufunguzi wa mafunzo ya siku tano kwa madaktari wa tiba ya viungo kutoka taasisi na vilabu vya michezo mbalimbali yaliyofanyika katika uwanja wa Uhuru.
Katika mafunzo hayo Profesa Mwansoko alisema lengo la mafunzo hayo ya siku tano ni kuwaongezea ujuzi wataalamu hao ili waweze kuwa na mbinu mpya zaidi katika utendaji wa kazi zao.
Aidha wataalamu hao pia wametakiwa kutumia mafunzo hayo kwa umakini kwani kwa kufanya hivyo watakuwa na nafasi ya kuwafundisha madaktari wengine ambao hawakupata nafasi ya kuhudhuria mafunzo hayo.
Wakati huo huo Daktari wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Antony Ngome alisema upungufu wa madaktari wanawake katika taaluma hiyo unachangia kwa kiasi kikubwa kudidimia kwa taaluma hiyo.
Mafunzo hayo yaliyoandaliwa kwa ushirikiano wa Serikali na Ubalozi wa Ujerumani nchini yanajumuisha washiriki 70 ambao wamegawanyika katika vituo vya Arusha na Dar es Salaam.





0 comments:
Post a Comment