Margreth Mkanga azindua kitabu cha "The Forgotten" HIV and disability in Tanzania

Mbunge wa viti maalum kwa upande wa walemavu Margreth Mkanga akiwa anazindua kitabu cha "The Forgotten" HIV and disability in Tanzania ambacho kimefanyiwa tafiti na TACAIDS kuhusiana na jinsi walemavu walivyosahaulika kwenye masuala ya ugonjwa wa UKIMWI wakati wa maadhimisho ya siku ya walemavu Duniani yaliyofanyika leo katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam. Aliyemshikilia kitabu hicho ni balozi wa Umoja wa Nchi za Ulaya (EU) nchini Tim Clarke.
Afisa Habari wa wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Catherine Sungura akionyeshwa kikapu na Sarah Namulondo ambaye ni mlemavu wa kutosikia wakati wa maadhimisho ya siku ya walemavu Duniani yaliyofanyika leo katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam. Walemavu hao kwa kupitia chama chao wanatengeneza bidhaa mbalimbali za mikono na kuziuza kwa wananchi na hivyo kujipatia kipato cha kila siku.


You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment