Uongozi wa timu ya Yanga leo umetangaza kuwatema rasmi wachezaji wake watatu, wawili kuwahamisha kwa mkopo na mmoja ambaye mkataba wake umekwisha katika klabu hiyo, akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya klabu hiyo mtaa wa Jangwani Afisa habari wa klabu hiyo Louis Sendeu amesema wachzaji walioachwa ni Khamis Yusuf, Mkenya james Shikokoti na mkenya mwingine Boniface Ambani.
Lous Sendeu ameongeza kuwa mchezaji Vicent Barnabas amehamishwa kwa mkopo kwenda katika klabu ya Africa Lione iliyoko chini ya Mbunge wa Singida Mjini Mohamed Dewji maarufu kama (Mo), kwa upande wa mchezaji Mike Baraza ambaye ni raia wa kenya Msemaji huyo wa Yanga amesema mchezaji huyo mkataba wake ulikwishamalizika katika timu hiyo ambayo ni bingwa mtetezi wa ligi kuu ya Vodacom japokuwa imekuwa ikisuasua katika mwenendo wa ligi kuu ya mwaka huu 2009 ambapo timu ya Simba inashika usukani kwa kujikusanyia pointi zote 33 katika mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo ikiwa imeshinda michezo zake zote
Mchezaji Mike Baraza katika siku za hivi karibuni ameripotiwa kwenda katika klabu ya Simba ya jijini Dar es salaam na hata yeye mwenyewe hajakataa wala kukubali kama kweli ameshasaini kuichezea timu hiyo ya mtaa wa Msimbazi katika mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom.
Kitu muhimu ni kusubiri wakati uongozi wa Simba utakapotangaza mchezaji gani mpya ataingia katika timu hiyo na mchezaji gani atahamishwa kwa mkopo kwani kocha mkuu wa timu hiyo mzambia Patrick Phiri amesema hayuko tayari kuacha mchezaji yeyote katika timu hiyo kwani karibu wote wana kiwango kizuri labda wanaweza kuhamishwa kwa mkopo tu kwenda kwenye klabu nyingine na kuongeza wachezaji wapya ili kuongeza nguvu kwa ajili ya mzunguko wa pili wa ligi kuu na mashindano ya kimataifa ya kombe la washindi.
0 comments:
Post a Comment