Mama Salma Kikwete.
Na Anna Nkinda - Maelezo, Mbeya
02/10/2009 Wanafunzi 2778 waliotarajiwa kufanya mtihani wa darasa la saba mwaka huu katika mkoa wa Mbeya hawakuweza kufanya mtihani huo kutokana na tatizo la utoro na mimba.
Hayo yamesemwa jana na Katibu Tawala wa mkoa huo Beatha Swai wakati akisoma taarifa ya Mkoa wa Mbeya kwa Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) aliyeko ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani humo.
Akitoa ufafanuzi wa idadi hiyo ya wanafunzi Swai alisema kuwa wanafunzi 78,429 walisajiliwa kufanya mtihani wa darasa la saba kwa mwaka huu lakini wanafunzi 2,778 ambo wavulana ni 1626 na wasichana 1152 hawakuweza kufanya mtihani huo.
Swali alisema, "Kati ya wanafunzi 2778 watoro ni 2626 ambao wavulana ni 1577 na wasichana ni 1049 na wanafunzi 39 walishindwa kufanya mtihani kwa ajili ya kupata ujauzito".
Taarifa hiyo pia inasema kuwa Mkoa wa Mbeya umepiga hatua katika upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi wake kwani hadi kufikia Septemba 2009 kiwango cha upatikanaji wa maji vijijini ni asilimia 59.9 na kamati za maji 523 zimeimarishwa kwa mafunzo na mifuko 352 imeanzishwa ambapo shilingi milioni 242.9 zimekusanywa kupitia mifuko hiyo.
Kwa upande wa mjini hadi sasa upatikanaji wa maji ni asilimia 93 sawa na masaa 22:15 kwa siku baada ya kukamilika ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya maji. Mkoa unazo Mamalaka Ndogo za Maji za makao makuu ya wilaya na miji midogo 10 zinazotoa huduma za maji.
Baada ya kupokea taarifa ya Mkoa Mama Kikwete aliongea na Wanawake wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) na kuwataka kupunguza mimba za utotoni pamoja na utoro kwa watoto wao kwani malezi ya watoto yako mikononi mwa wanawake, wanaume wanachofanya ni kuwasaidia tu.
Alisema kuwa idadi ya wanafunzi watoro pamoja na wanaopata ujauzito ni kubwa sana hivyo wao kama wazazi wanatakiwa kuongea na watoto wao ili wabadilike kitabia na kupunguza taizo hili au kama itawezekana kuliondoa kabisa.
"Inasikitisha sana kuona kuwa watoto wetu wanashindwa kumaliza shule kutokana na tatizo la utoro na mimba kwani kama wangweza kumaliza masomo yao wangepatikana wataalamu mbalimbali ambao wangeweza kuleta maendelea ya nchi yetu na hivyo kupunguza tatizo la wataalamu tulilokuwa nalo hapa nchini", alisema Mama Kikwete.
Mwenyekiti huyo wa Taasisi ya WAMA aliendelea kusema kuwa tatizo hili kama halitaweza kutatulia hali ya umaskini haitaweza kupungua katika jamii ya kitanzania kwani kutakuwa na maisha ya kutegemeana kwa kuwa watoto wengi hawatakuwa wamepata elimu ya kutosha ambayo itawasaidia kuinua kiwango chao cha maisha kwa kupata ajira Serikalini na katika Sektabinafsi.
Mama Kikwete aliwakabidhi kadi za uwanachama wa UWT wanachama wapya watano kwa niaba ya wenzao 150 ambao ni wanafunzi wa vyuo vikuu vishiriki vilivyopo katika mkoa huo.
Taasisi ya WAMA ilikichangia Chama cha Kuweka Akiba na Kukoba (SACCOS) cha Mbeya City Women Group ambayo inamilikiwa na UWT, Tshs.1,500,000/= fedha ambazo zitatumika kuinua mtaji wa chama hicho.

0 comments:
Post a Comment