Tanzania yajitutumua tena kwenye maonyesho ya Utalii nchini Uingereza!

Mh. Shamsa Mwangunga katikati akiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa Utalii nchini waliohudhuria katika maonyesho hayo.
Tanzania imefanikiwa kufanya vyema tena kwenye maonyesho ya Utalii yaliyofanyika nchini Uingereza mwanzoni mwa mwezi huu, Tanzania kwa mara nyingine imeshiriki kwenye maonyesho ya hayo kuanzia tarehe 9 mpaka tarehe 12 November 2009,
Bodi ya Utalii nchini (TTB) ndiyo iliyosimamia kikamilifu ushiriki wa Tanzania klatika maonyesho hao makubwa na maarufu nchini Uingereza, Banda la Tanzania lilikuwa ndiyo kati ya mabanda mazuri na ya kuvutia kati ya nchi washiriki zilizoshiriki kwenye maonyesho hayo.
Jumla ya kampuni binafsi 59 kutoka Tanzania zilikuwepo kuuza vivutio vya Utalii na safari kwa wageni ili kutembelea na kufanya utalii nchini Tanzania, Ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Shamsha Mwangunga na baadhi ya maafisa wengine kutoka Tanapa, Ngorongoro na Bodi ya Utalii waliowakiliswa na Mkurugezi Mkuu wa Bodi hiyo Mr. Peter Mwenguo.
Nchi ya Tanzania imeweza kutangazwa kupitia maonyesho hayo makubwa duniani yajulikanayo kama World Traveller Market (WTM) yaliyofanyika katika viwanja vya excel jijini London nchini Uingereza

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment