Rwanda wapata wawakilishi Miss East Africa 2009!!

Fimbo tatu za Rwanda: Miss East Africa Rwanda, Cynthia Akazuba (aliyeketi) akiwa na mshindi wa pili, Annete Mahoro na mshindi wa tatu, Sabrina Kangezi mara baada ya kutawazwa washindi
Na mwandishi wetu, kigali
MISS Kigali , Cynthia Akazuba juzi usiku aliibuka mshindi katika shindano la kumsaka Miss East Africa Rwanda baada ya kuwashinda warembo wengine 11.
Katika shindano hilo lililofanyika kwenye hoteli ya Serena mjini hapa, Cynthia alizawadiwa faranga milioni moja karibu sh milioni tatu za kitanzania.
Kwa ushindi huo sasa Cynthia ataiwakilisha Rwanda katika fainali za Miss East Africa zitakazofanyika Desemba 18 kwenye ukumbi wa Mlimani City , Dar es Salaam .
Mrembo Annete Mahoro alishika nafasi ya pili akiondoka na faranga 500,000 sawa na karibu milioni moja na nusu ya Tanzania . Annete pia ataiwakilisha Rwanda kwenye fainali za Miss East Africa.
Nafasi ya tatu ilikwenda kwa Sabrina Kaganza wakati Viviane Umulisa na Ritha Uwera walishika nafasi ya nne nay a tano. Majaji wa shindano hilo Rena Callist, Petter Mwendapole ( Tanzania ), Lauren Makuza na Evelyne Umurerwa ( Rwanda ) na Inamahoro Chantal ( Burundi ) walimchagua mrembo Uwera Magreth kuwa Miss Photogenic na vazi zuri la ubunifu ambapo alipata ofa ya kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii Tanzania pamoja na kuishi kambini na warembo wengine wa Miss East Africa .
Shindano hilo lilipambwa na wasanii mbalimbali wa Rwanda lakini muigizaji Ntarindwa Diogene alionekana kukongoka nyoyo za mashabiki waliohudhuria onyesho hilo . Pia mwanamuziki Meddy alichangamsha onyesho hilo .
Warembo wote 12 walipita jukwaani na mavazi ya ubunifu, jioni vazi la asili kabla ya kuchujwa na kubaki watano ambao waliulizwa maswali mbalimbali kuhusu Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na maisha yao binafsi.
Kambi ya Miss East Africa itakuwa Kunduchi Beach Hoteli na itaanza Desemba 1 mwaka huu.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment