PAPIC AREJEA, KUANZA KAZI YA KUKINOA KIKOSI CHAKE LEO JIONI!!

Kostadian Papic kocha wa timu ya Yanga.

Kocha mkuu wa Timu ya Yanga mserbia Kostadian Papic amewasili leo asubuhi kwa shirika la ndege la KLM tayari kwa kuanza kazi ya kukinoa kikosi chake kwa ajili ya mashindano ya kombe la Tusker na mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom hapo baadae itakapoanza.
Akizungumza na FULLSHANGWE Afisa habari wa Timu hiyo ya mtaa wa Jangwani Bw. Louis Sendeu amesema kocha mkuu Papic ameshatua leo hii asubuhi na mazoezi yanaanza mara moja leo jioni kwenye uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam.
Sendeu amesema kambi imeanza mara moja ili mwalimu aendelee vyema na programu yake ya kukiweka sawa kikosi cha Yanga, ili kuwa tayari kwa kukabiliana na mashindano yoyote ambayo yako mbele hasa tukianzia na Kombe la Tuske.
Awali Kocha Kostadian Papic ambaye alikuwa nyumbani Serbia kwa mapumziko mafupi akiwa huko wiki iliyopita, alieleza kuwa atarejea mara moja nchini ili aweze kuanza kazi ya kukinoa kikosi chake, na akaongeza kuwa hatahitaji visingizio vyovyote kutoka kwa wachezaji watakaoonekana kutega kwenye mazoezi kwani kila mchezaji anayo sababu ya kufanya kazi kwa kwa bidii na kujituma kama alivyoyakubali jukumu la kuitumikia timu.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment