Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Ezekiel Maige kulia akiongea na wanahabari katika makao makuu ya Wizara hiyo leo wakati alipozungumziamabadiliko ya tarehe ya upandaji miti ambayo ilikuwa ikifanyika kila mwaka Januari mosi na kuwa Aprili mosi kutokana na mabadiliko ya waraka wa Waziri mkuu na. 1 wa mwaka 2009 kuhusu kubadili siku ya kupanda miti kutoka January Mosi na kuwa Aprili Mosi kila mwaka rasmi kuanzia mwaka kesho.Wakati huohuo kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dr.Ladslaus Komba imesema Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya muungano Mh. Pius Msekwa kuwa Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa mamlaka ya Hifadhi ya Ngorogoro (NCAA)
Na Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Shamsa Mwangunga amewateuwa wajumbe wa bodi ya Mamlaka hiyo ambao watasaidiana na mzee Msekwa ni Mh. Job Y. Ndugai Mbunge wa Kongwa, Bw. Metui Ole Shaudo- Mwenyekiti Baraza la Wafugaji ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara na kilimoTanzania, Mh. Lucas Selelii -Mbunge Nzega, Mh. Halima Mamuya -Mbunge Viti maalum Arusha na Bw. Emmanuel Lomayani -Mwakilishi wa wafanyabiahara wa mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro, Bw. Donatius Kamamba- mkurugenzi idara ya mambo ya kale Wizara ya Maliasili na utalii, Bw. Deogrtias Ntukamazina- Katibu mkuu Mstaafu Utumishi, Bw. Yona Nko wa ArushaBw. George Kaindoh - Mshauri Mwelekezi, Mjumbe kutoka Jeshi la Polisi na Bw. Bernard Murunya - Mhifadhi mkuu hifadhi ya Ngorongoro kuwa Katibu wa bodi hiyo katika picha kushoto kwa Naibu Waziri ni Felician Kilahama Kaimu Katibu Mkuu na mkurugenzi wa misitu na nyuki.





0 comments:
Post a Comment