ELIZABETH GUPTA AONGEA NA WAANDISHI WA HABARI!!

Aliyekuwa mshiriki wa Bigbrother Revolution Elizabeth Gupta akiongea na wanahabari sasa hivi katika mkutano unaoendelea kwenye Hoteli ya Paradise City jijini Dar es salaam, Elizabeth alirejea jana kutoka afrika Kusini baada ya kuishi katika jumba hilo kwa siku 63 na baadaye kupigiwa kura ya kutoka nje na washiriki wa shindano hilo pamoja na mashabiki,
Elizabeth amesema anashukuru kwa kupata nafasi hiyo kwani amejifunza mambo mengi lakini pia anaweza kupata mafanikio mengine mengi kutokana na ushiriki wake katika shindano la Bigbrother Revolution na anaamini kwamba wasichana wengi watakuwa wamejifunza mengi kupitia kwake pia ameomba radhi kama kuna mashabiki aliwaudhi kwani katika maisha ya kila siku kwenye jumba hilo sio rahisi kumfurahisha kila mtu.
Meneja Huduma wa Multchoice Ronald Shelukindo akizungumza na wanahabari wakati wa kumkaribisha Elizabeth Gupta katikati ili aongee na wa aandishi wa habari katika mkutano unaoendelea kwenye Hoteli ya Paradise City jijini Dar mara baada ya kurejea jana kutoka Afrika kusini.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment