China imewanyonga watu wawili waliotiwa hatiani katika kashfa ya maziwa ya unga yaliyosababisha vifo vya watoto sita.
Zaidi ya watoto wengine 300,000 waliugua baada ya kutumia maziwa hayo ya unga yaliyokuwa yamechanganywa na kemikali inayotumiwa kutengeneza mbolea na bidhaa za plastiki.
Zhang Yujun na Geng Jinping ndio watu pekee walionyongwa kuhusiana na kashfa hiyo.
Washtakiwa wengine kumi na tisa walihukumiwa vifungo vya jela.
Zhang Yujun alishtakiwa kuhatarisha afya ya umma kwa kutumia njia hatari baada ya kuuza zaidi ya tani 770 za maziwa hayo ya unga kuanzia mwezi Julai mwaka 2007 hadi mwezi Agosti mwaka 2008.
Geng Jinping, aliyekuwa akisimamia uzalishaji wa maziwa hayo, alitiwa hatiani kwa kusambaza maziwa hayo kwa kampuni ya Sanlu Group ambayo sasa imefilisika, pamoja na kampuni nyingine za maziwa.
Watu hao walihukumiwa mwezi Januari huko Shijiazhuang, mji mkuu wa Hebei, ilipokuwa makao makuu ya Sanlu. Rufaa yao ilitupwa na mahakama kuu ya Hebei mwezi wa Machi.

0 comments:
Post a Comment