BUSTER RHYMES AFANYA KWELI FIESTA 2009, AMKUBALI CHID BENZ!

Buster Rhymes kulia akimfariji Mkurugenzi wa Clouds Media Group Joseph Kusaga aliyenyanyua mkono juu, kutokana na kuondokewa na baba yake mzazi Marehemu Mzee Alex Kusaga ambaye ndiye alikuwa mwenyekiti wa kampuni hiyo mara baada ya kufanaya onyesho la kukata na shoka usiku wa kuamkia leo kwenye viwanja vya Posta Jijini Dar es salaam, Busta alifanikiwa kuziteka nyoyo za mashabiki kwa kiwango cha juu huku akisifu Tanzania na watu wake akisema ni watu wazuri wakarimu na akasema anafurhishwa sana na umati wa mashabiki uliokuwa umejitokeza kwenye tamasha hilo la Fiesta One Love 2009.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Clouds Media Group Joseph Kusaga alisema anamshukuru sana Buster Rhymes kwa kujali na kuwa na moyo wa huruma kwani onyesho hilo lilikuwa lifanyike Novemba 7 likaahirishwa kutokana na msiba huo hata hivyo Buster Rhymes alikubali kuja kufanya onyesho Novemba 21 pamoja na kazi zake nyingi akamshukuru sana na akasema onyesho hilo analitoa kama Dedication kwa Marehemu baba yake.
Buster Rhymes kulia akiwa na mkali mwingine aliyeongozana naye, huyu si mwingine ni Splifstar aliyeko kushoto wakiwadatisha mashabiki katika viwanja vya Posta Kijitonyama usiku wa kuamkia leo.
Mkali Buster Rhymes Jukwaani sasa! alistaajabu umati wa watu ulivyokuwa mkubwa na akasifu sana Tanzania na watu wake.
Hapa ndipo Buster Rhymes alipompa pongezi Chid Benz kabla hajapanda jukwaani kwa Swaga lililofunika Fiesta One love 2009 kwa wasanii wa bongo.
Mabaunsa walikukuwa na kazi ngumu baada ya uzalendo kuwashinda mashabiki na kutaka kuvamia jukwaa kutokana na hisia walizokuwa wakipata wakati Buster Rhymes anafanya mambo makubwa.
Msanii Pekee wa Tanzania Chid Benz aliyefanikiwa kuteka hisia za Buster Rhymes wakati akighani jukwaani, alifanya onyesho la kukata na shoka na alikuwa na nguvu za kucheza na kuimba wakati wote alipokuwa jukwaani, hongera Chid Benz.
Mashabiki kunyanyua juu mikono Hii haikuwa amri bali ilikuwa burudani tu.
Adam Mchomvu wa Clouds Radio kulia akiongoza burudani kwa mashabiki chini ya jukwaa.
Akudo Impact wao wakaonyesha shoo kivyao chini ya jukwaa, iilikuwa kali sana staili yao.
Huyu ndo yule mkali wa kurap anaitwa Cpwaa.
(HBC) Unawakumbuka hawa jamani mdau nao walikamua kikamilifu kuoka kulia ni Prof. J, Willy, na Terry enzi hizo wakijulikana kama kundi la Hardblasters.
Ikawa ni zamu ya Marlow kufanya vitu vyake.
Naye mzee wa mitulinga Profesor J. akakamua vilivyo katika jukwaa hilo la Fiesta One Love.
Vijana wa kazi THT wakiwajibika nadhani kwa sasa hawana mpizani jijini Dar es salaam.
Wakati wenzie wanaserebuka na Buster Rhymes yeye Farida hali ilikuwa mbaya sana maana alikuwa amebanwa kwenye kona ya vyuma hata muziki ulikuwa haupandi kabisa.

Witness akiwa amepagawa na mzee mzima Buster Rhymes ilikuwa si mchezo!

Chui wa Serengeti wafalme wa raha kamili wao ni rafiki wa kila mtu kama unavyoona wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya bia ya Serengeti.
Kutoka kulia ni Sizzy Azizi wa B. Band, Bazo Komu wa TBC1, Nelly , Babla, Abuu meneja wa B. Band na Banana Zorro kiongozi wa B. Band nao walikuwepo kwenye tamasha la Fiesta One Love usiku wa kuamkia leo.
Meneja matukio na promosheni wa Serengeti Breweriers Bahati Singh katikati akionyesha One Love kwa Maunda Zorro kushoto na Baby Madaha.

Frolenso na Debora Nyangi wa Kalunde Band wakashow nao One Love ya Fiesta
Chui wa Serengeti wakawa rafiki wa Meneja uhusiano wa Serengeti Breweriers Teddy Mapunda,
Gardiner G. Habash kama Kapteni wa Jahazi alikula kivazi hiki.
Baby Madaha katika pozi! unalionaje mdau.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

1 comments:

  1. Sasa huyo bouncer anamkinga Chid Benz kwanini? hawa ma-bouncer wetu watu wa ajabu sana Busta anataka kumpa mkono kijana anamsukuma? Hizi protocol za kazi hii tunazizidisha

Post a Comment