Fatma Amour amefanya mambo makubwa huko Marekani katika maonyeho ya mavazi yanayoendana na mafunzo ambapo Wanawake watanzania 13 wako nchini humo kwa mafunzo mbalimbali ya kazi za sanaa kwa mwezi mmoja, hili ni kundi la tatu kwenda nchini Marekani kwa mafunzo hayo makundi mengine mawili yameshakwenda na kupata mafunzo na wamerejea nchini.
Wanawake wasanii hao wanatoka mikoa ya Tanga, Zanzibar, Dar es salaam Arusha na Dodoma na Wilaya ya Bagamoyo wameendelea kushiriki katika maonyesha ya sanaa za aina mbalimbali yanayoandaliwa na vikundi vya sanaa vya Jimbo la Ohio nchini humo.
mafunzo yalianza tarehe 6 oktoba na yatamalizika tarehe 3 Novemba ambapo mpango huu wa mafunzo unadhaminiwa na serikali ya Marekani, wasanii hawa pia watatembelea jumuiya mbalimbali katika majimbo ya Michigan na Ohio,
Katika safari hiyo Mwanamitindo mbunifu wa Tanzania Fatma Amour Hamad wa Famour Designs amefanya mambo makubwa katika maonyesho na amezindua mitindo yake katika hafla ya uchangiaji wa sanaa yenye jina "Magic Of Tanzania" uzinduzi umefanyika jimbo la Ohio oktoba 12, katika uzinduzi huo pia pia ametambulisha na ataendelea kutambulisha mitindo na kazi zake nyingine za sanaa katika maonyesho mengine yanayoendelea sambamba na mafunzo yao nchini humo.
Fatmar Amour katikati akiwa na wanawake wenzie na wadau mbalimbali wa sanaa nchini humo.
0 comments:
Post a Comment