MAMA's with Zain awards na matukio katika picha!!

Mwanamuziki AY akisalimiana na mashabiki wa muziki mjini Nairobi alipokuwa kwenye tuzo za Zain MTV Music Award zilizofanyika mwishoni mwa wiki, AY alikua mmoja wa washindani katika upande wa Hiphop ambapo Amani kutoka nchini Kenya aliibuka mshindi wa tuzo hiyo
Shaa akiwa anahojiwa na waandishi wa habari muda mfupi kabla ya kuingia katika tuzo za MTV Music Award zilizofanyika nchini Nairobi Kenya mwishoni mwa wiki

Mwanamuziki wa kizazi kipya anayekuja juu nchini Tanzania Shaa akisalimiana na wapenzi wa muziki alipokuwa kwenye tuzo za MTV Music Award Nairobi Kenya mwishoni mwa wiki.Shaa alikua mmoja wa wanamuziki aliechaguliwa kushindania tuzo hiyo ambapo mwanamuziki Dibanj kutoka Nigeria aliibuka mshindi.



You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment