TAIFA QUEEN YAWANYANYASA LESOTHO KATIKA NETBALL!!

Mke wa Rais Mama Salama Kikwete aliyekuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mashindano ya netball kwenye uwanja mkuu wa Taifa jana akisalimiana na wachezaji wa timu ya taifa ya Lesotho kabla ya kuanza kwa mchezo kati ya Tanzania na Lesotho ambapo Tanzania ilishinda magoli 33-19 mashindano hayo ya kimataifa ya Netball yanasimamiwa shirikisho la vyama vya Netball vya kimatifa International Federation of Netball Association (IFNA)
Mchezaji wa Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Queen akijaribu kufunga goli katikati ya walinzi wawili wa timu ya Lesotho wakati wa mchezo wa kwanza wa ufunguzi wa mashindano hayo ya Mchezo wa Netball kati ya timu hizo iliyofanyika jana kwenye uwanja mkuu wa taifa Tanznia ilishinda magoli 33-19.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake wakati alipofungua mashindano ya Netball kwa nchi za Afrika yanayofanyika nchini yakiandaliwa na chama cha Netball CHANETA yaliyoanza jana kwenye uwanja mkuu wa Taifa. kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Evance Balama na anayefuata ni Anna Bayi Mwenyekiti wa Chama cha hicho.
Kuazia kushoto ni Timu za Tanzania, Namibia na Afrika kusini zikiwa zimekaa tayari kwa kupigiwa nyimbo za mataifa yao wakati wa ufunguzi wa mashindano ya NetBall kwa nchi za Afrika jana kwenye uwanja mkuu wa Taifa.
Timu mbalimbali zikiwa zimejipanga tayari kwa kudigiwa nyimbo zao za Taifa

Kikundi cha ngoma cha JWTZ kikitumbuiza wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo yanayoshirikisha nchi mbalimbali za Afrika.
Katibu mkuu msaidizi wa CHANETA Rose Mkisi kushoto na Mweka hazina wa chama hicho Flora Kasambara wakiingia katika viwanja vya mashindano kabla ya kufunguliwa rasmi na mke wa rais Mama Salma Kikwete jana.
Wanafunzi kutoka shule mbalimbali walihudhuria katika uzinduzi wa mashindano ya Netball kwa nchi za Afrika yaliyozinduliwa jana kwenye uwanja mkuu wa Taifa jijini Dar se salaam.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment