Meneja wa kinywaji cha Redds Kabula Nshimo akikabidhi begi kwa mmoja wa washiriki wa Vodacom Miss Tanzania kutoka Mwanza Bagi la safari Redds ilikabidhi mabegi ya safari kwa washiriki wote wa shindano hilo.Meneja wa kinywaji cha Redds kinachozalishwa na Tanzania Breweries Ltd Kabula Nshimo akizungumza na waandishi wa habari katika kambi ya Vodacom Miss Tanzania iliyopo kwenye Hoteli ya Girrafe Ocean View Kunduchi kuelezea jinsi shindano la Redds Miss Photogenic litakavyoendesha.
Amesema warembo wanaoshiriki shindano hilo watatakiwa kubuni jinsi ya kupiga picha zao wenyewe ambazo zitapigiwa kura na wadau mbalimbali wa urembo likiwemo jopo la wapiga picha na kura hizo zitaendeshwa kupitia Blog ya http://www.issamichuzi.blogspot.com/ ambako picha za warembo wote zitapatikana humo na kupigiwa kura ili kumpata mshindi wa shindano hilo TBL ni wadhamini wenza wa Vodacom katika shindano la Vodacom Miss Tanzania kupitia kinywaji chao cha Redds





0 comments:
Post a Comment