Waziri George Mkuchika.
(Na Benjamin Sawe – Maelezo – Newala)
Serikali imetoa kiasi cha Shilingi Milioni 800 na kununua pampu za kusukumia maji katika wilaya ya Newala kwa lengo la kukabiliana na tatizo la maji katika wilaya hiyo. Hayo yamesemwa jana na Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo ambaye pia ni Mbunge wa Wilaya ya Newala, Mheshimiwa George Mkuchika wakati wa ziara yake ya siku tano ya kutembelea Wilaya hiyo.
Mhe. Mkuchika amesema, kugundulika kwa gesi katika kijiji cha Msimbati mkoa wa Mtwara kutasaidia kwa kiasi kikubwa kupatikana kwa umeme wa uhakika na kwamba Serikali ipo katika hatua za awali za kuhakikisha kuwa umeme wa uhakika unapatikana katika wilaya hiyo kwani bila umeme maji yasingepatikana. Akizungumzia suala la elimu katika wilaya ya Newala, Mhe. Mkuchika amesema, jumla ya shule 26 zimejengwa katika wilaya yake na kuvuka lengo la awali lililowekwa la kujenga shule 22.
“Tulikuwa na lengo la kujenga shule 22 katika wilaya ya Newala lakini tumejenga shule 26 hivyo tumevuka lengo katika wilaya yetu kwa kujenga shule nne zadi,” alisema Mkuchika. Aidha Mheshimiwa Mkuchika amesema, Serikali imeanzisha mfumo wa stakabadhi ghalani na kusema mfumo wa zamani ulikuwa unawadhulumu na kuwakandamiza wakulima. Katika mfumo uliokuwepo, wamekuwa wakidhulumiwa haki yao kwani wanunuzi walikuwa wakijipangia bei kutokana na matakwa yao hivyo kupelekea wakulima kukosa haki zao. Katika ziara hiyo alitembelea vijiji vya Mapili, Mkunya, Mitumbatu na Chihwindi ili kujionea maendeleo mbalimbali. Mheshimiwa Mkuchika pia ametembelea chanzo cha maji cha Nkunya katika wilayaya Newala. Mhe. Mkuchika amesema, kwa kushirikiana na Serikali vyama vingi vya Ushirika vimeweza kujenga ofisi zao na kununua gari la wagonjwa katika hospitali ya Newala.
“Tukiendelea kushirikiana hivi kwa miaka kumi Wilaya yetu ya Newala itafika mbali na kuwa na maendeleo kupita Wilayazote katika Mkoa wa Mtwara.” Wakati huo huo Mheshimiwa Mkuchika amewaasa wananchi wa Wilaya ya Newala kuacha tabia ya kutembea na wanafunzi kwanikwa kufanya hivyo wanawanyima haki lililowekwa yao ya msingi ya kupata elimu.Alisema. Pia alisema kuwa kwa sasa Serikali ina mpango wa kujenga kituo kikubwa na cha kisasa cha polisi katika wilaya hiyo ili kuendelea kudumidha ulinzi na amani katika wilaya ya Newala. Pia Serikali imetoa zaidi ya shilingi milioni miasita kwaajili ya matengenezoya barabara za wilayani pamoja na barabara ya kuingia mjini Newala.
0 comments:
Post a Comment