KATIBU MKUU MALI ASILI NA UTALII MGENI RASMI VODACOM MISS TANZANIA IJUMAA!!

Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundenga leo katika katika ofisi ya kamati hiyo mtaa wa mkwepu jiji Dar ametangaza Mgeni rasmi katika shindano la Vodacom Miss Tanzania 2009 linalotarajiwa kufanyika ijumaa hii oktoba 2 kwenye ukumbi wa Mlimani City.
Akizungumza na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali Hashim Lundenga amesema katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dr. Ladislaus Komba ndiye atakuwa mgeni rasmi katika shindano hilo lenye mvuto wa hali ya juu nchini, Lundenga ameongeza kuwa Dr. Ladslaus Komba ni mtu muhimu kwa shindano letu kwa kuwa shindano la Miss Tanzania pia linatangaza utalii wa nchi yetu, hivyo kuwepo kwake katibu mkuu huyo wa Wizara ya Maliasili na Utalii kutaamsha zaidi ari ya watanzania kujitokeza katika kuutangaza na kuuthamini utalii wa nchi yetu.
Wakati huohuo Lundenga amewataja majaji watakaoamua na kmpata mrembo wa Tanzania siku hiyo, amesema walipeleka majina 15 kwenye Baraza la sanaa nchini ili wapatiwe majaji watakaochagua mrembo wa Tanzania, na Baraza la Sanaa BASATA limewarudishia majina 9.
Ameyataja majina hayo na sehemu wanazotoka kuwa ni Bw. Robert Collmore Mjumbe wa Bodi ya Vodacom kutoka Vodafone Uingereza, Suzan Mungi Mkurugenzi wa Habari na Matukio Shirika la Habari Tanzania TBC,Dorris Malulu Afisa Uhusiano Kampuni ya bia TBL, Devotha K. Mdachi Mkuu wa Kitengo cha Habari na Utalii, Capt Sadiki Muze Rubani shirika la ndege ATCL, Lusekelo Mwakalukwa Corporate Governace Manager Tanzania One, Bernad Mrunya Mhifadhi Mkuu Hifadhi ya Ngorongoro NCAA, Stella G. Kariuki Afisa Utawala Kampuni ya Simu SAMSUNG na Prashant Patel Mwenyekiti Kamati ya Miss Tanzania.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment