EAST AFRICAN BREWERIES YAJENGA JENGO LA KITENGO CHA MACHO KCMC HOSPITAL!!

Jengo la kitengo cha macho linalojengwa katika Hospitali ya KCMC Moshi.

Kampuni ya bia ya East African Breweries Limited EABL iliyoko nchini Kenya imejenga kitengo cha huduma ya macho katika hospitli ya rufaa yaKCMC ambacho kitagharimu zaidi ya shilling million 150 hadi kukamilika.Akizungumza wakati wa kukagua ujenzi wa jingo hilo Mkurugenzi wa Idara ya huduma wa kampuni hiyo bwana Ken Kariuki alisema kampuni hiyo iliamua kujenga kitengo hicho baada ya kufika katika hospitali hiyo na kukuta haina kitengo cha macho.

Bwana Kariuki alisema jingo hilo ambalo limeanza kujengwa miaka miwili iliyopita wanatarajia kulimaliza mwezi octoba mwaka huu na watalikabidhi kwa wahusika ili wananchi wa moshi na maeneo jirani ya nje na ndani ya nchi waweze kunufaika na huduma yamachoKampuni yetu hujishughulisha sana na mambo mbalimbali ya kusaidia jamii ikiwa ndio njia mojawapo ya kurudisha faida tunayoipata kutoka kwa wananchi, na ndipo tulipoamua kuja kuuliza wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro kuwa wanahitaji nini na walisema wanakabiliwa na tatizo la kitengo cha macho katika hospitali hiyo, alisema Bwana Kariuki.
Katika ukaguzi wa mradi huu alikuwepo pia Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Bibi Monica Mbega naye aliishukuru sana kampuni hii ya bia ya Africa Mashariki kwa kuwa mbele kuisaidia jamii kwa kujenga wodi ya macho nakuendeleza miradi ya maji kama vile ule mradi wa Mkuranga ambao umeigharimiwa na EABL kwa kiasi cha million 350 na mradi huu umeweza kusaidia zaidi ya kata 11 na watu zaidi ya 300,000 wamefaidika.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment