BREAKING NYUUUUZ, MCHEZAJI WA MPIRA MIGUU "SAID MHANDO" KATUTOKA!!

Mchezaji Saidi Mhando aliyewahi kuchezea timu za Coastal Union ya mkoani Tanga, Timu ya Simba ya jijini Dar es salaam na hatimaye Yanga pia ya jijini Dar es salaam amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Amana ya jijini.
Habari zilizotufikia kutoka kwa watu wa karibu na mchezaji huyo wa zamani aliyechezea timu hiyo zaidi ya miaka mitano iliyopita zinasema mpaka sasa msiba uko nyumbani kwao Magomeni Kota ambako ndiko wazazi wake wanaishi,
Marehemu Saidi Mhando atasafirishwa kesho kwenda kijijini kwao Kisarawe ambako pia mama yake mzazi ndiko alikozikwa, mazishi ya mchezaji huyo yanatarajiwa kufanyika saa kumi jioni mara baada ya kuwasili huko.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment