WAISLAMU NCHINI WATAKIWA KUACHA MAOVU!!

Waziri mkuu Mh. Mizengo Pinda kulia akisalimiana na Waziri wa Kazi Ajira na Vijana katika moja ya matukio waliokuwa pamaoja.

Na Anna Nkinda - MaelezoDar-Es-Salaam
Waislamu nchini wametakiwa kutenda matendo yaliyo mema na kujiepusha na maovu katika maisha yao ili waweze kupata thawabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Wito huo umetolewa hivi karibuni na Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana Prof. Juma Kapuya wakati akiongea na Waislamu wa Mkoa wa Dar es Salaam katika kongamano la kuukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhani lililofanyika viwanja vya Mnazi Mmmoja. Waziri Kapuya ambaye alikuwa ni mgeni rasmi katika kongamano hilo aliwataka waislamu hao pia kufuata nguzo tano za imani yao ambazo ni kutoa shahada, kusimamisha swala, kufunga mwezi wa Ramadhani, kutoa zaka na kwenda kuhiji Makka kwa wale wenye uwezo. "Watukufu Waislamu ninachosema hapa ni kwamba binadamu ameumbwa, ataishi, atakufa, atafufuka, atahukumiwa na baada ya hapo ataishi katika raha au mateso kutokana na vitendo vyake hapa Duniani hivyo basi ni wajibu wenu kuishi kadri ya neno la Mungu linavyosema", alisema. Akiongelea umuhimu wa kufunga wakati wa Mwezi wa Ramadhani Waziri Kapuya alisema kuwa kufunga ni amri na lazima kwa kila muislamu kama Mwenyezi Mungu anavyosema katika aya ya 183 ya Surat Al-Bakara.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment