Cliford Ndimbo wa pili kutoka kushoto ambaye tayari amelamba dume kama afisa habari wa Timu ya Simba, Je vipi wanahabari wengine nao watatokaje? wa kwanza kushoto Baruan Muhuza,watatu Juma Nkamia, Evance Mhando na Enock Bwigane, picha hii ilipigwa tarehe 26/ March 2008 siku ya uzinduzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Mikocheni jijini Dar es salaam.
Kulia aliezibwa na Camera ndie Louis Sendeu akiwa anava microphone akijianda kumuhoji mchezaji wa mpira wa Kikapu wa Kitanzania anaecheza huko nchini Marekani kwenye ligi ya NBA Hasheem Thabeet kwenye kipindi cha kila wiki cha Michezo cha kwenye Luninga kinachoitwa MEZA YA MICHEZO kinachorushwa na Television ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) inayoitwa TBC1 hapo August 16/ 2009.Hii leo jumamosi 22 August 2009 baada ya kupita wiki moja Louis Sendeu ametangazwa na timu ya ligi kuu Tanzania bara ya YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB (YANGA) kuwa msemaji wa timu hiyo ikiwa siku moja kabla ya kuanza kwa ligi kuu Tanzania bara msimu mpya wa 2009 - 2010.Yanga ni miongoni mwa timu zilizochelewa kutimiza azimo la Bagamoyo la kila timu za ligi kuu Tanzania bara kuanzi msimu huu wa 2009 - 2010 kuwa na watendaji watu wa kuajiliwa.Mwingine alieula Yanga ni mchezaji wa zamani wa timu hiyo ya Yanga Lawrence Mwalusako ambae yeye amekuwa katibu mkuu na mtunza pesa ni Godfrey Mwenje.Sendeu anakuwa mwandishi na Mtangazaji wa pili toka Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kuwa msemaji wa timu ya ligi kuu wa kwanza alikuwa ni Cliford Ndimbo aliechukua cheo kama hicho kwenye timu ya Simba.Kila la heli mwanahabari mwenzetu Louis Sendeu katika ajira nyingine pamoja na Cliford Ndimbo.
0 comments:
Post a Comment