Mtanzania Teddy Kalonga kwa mara nyingine tena anabeba bendera yetu, tumpigie kura!!


Mtanzania Teddy Kalonga kwa mara nyingine tena anabeba bendera yetu ughaibuni na hivi sasa amekuwa ni mmoja wa warembo wanaowania nafasi ya kuwa mtangazaji Luninga ya SPIKE TV.
SPIKE TV ni channel ya Michezo ya wanaume huko Marekani.
Teddy anatakiwa kupigiwa kura ili ashinde nafasi hiyo ambayo mwenyewe anasema hajawahi kuifanya maishani na anafurahi akiipata na kuahidi kulitangaza vyema jina la Tanzania.

“well, nilienda kufanya interview sikujua kama kutakuwa na mambo ya picha au competitions, ila ndio hivyo nimekuwa mmoja wa washindani” alisema Teddy alipoongea na Spoti Starehe leo. aidha nilimuuliza Teddy kama Channel hiyo inahusika na mambo gani ni michezo tuu ama naye alisema”…mambo mengi kama the most shocking reality things, cars, I mean vitu vingi vinavyopendwa na wanaume mostly”.
Piga kura yako hapa http://www.spike.com/spike-girl/500960

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

1 comments:

  1. Mhhh mweee…jamani mie rabda mshamba, sasa ni waulize
    Kuna uhusiano gani kati ya utangazaji wa tv na kupiga picha za uchi??? Mhh mbona hii ya dada yetu Teddy haina tofauti na lile shindano la “PLAY BOY”! Jamani twendeni mbele na kurudi nyuma, njaa itatufikisha kubaya, tumefikia hatua yakuuza utu wetu kwa tu dola tu? Hee nimeingia huko ULTIMATE SPIKE GIRL nkamuona dada yangu TEDDY sikuweza kuendelea. Ni uchi wa mnyama kabisaaaa! Wale wengine siwezi kuwalaumu pengine Tamaduni zao zinakubali! Lakini kwa ndugu yetu Teddy this is tooooooooooooo much!

Post a Comment