HI wadau mnipeperushie hii tukiwa tunajiandaa na mwezi huu mtukufu (Shamimu Zeze)

Ndugu wapendwa, mwezi mtukufu ndo huu umewadia, leo ni Shaaban Chungu 15, kama alivyosema Allah (SW) katika Surat Baqarah: - (183, 184, 185)

185. ''Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur'ani kuwa ni uwongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uwongofu na upambanuzi. Basi ataye kuwa ameona mwezi naafunge. Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi atimize hisabu katika siku nyengine. Mwenyezi Mungu anakutakieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo mazito, na mtimize hiyo hisabu, na mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa kuwa amekuongoeni ili mpate kushukuru.''

Basi ndugu zanguni, mtapata kufahamu Zaidi Falsa ya Swaumu kutoka katika DVD ya Ustaadh Kondo J. Bungo itakayokuwa mitaani wiki ijayo Inshaallah. Usiache kujipatia copy yako ili uweze kuanza kudodosa wewe na familia.
Mpango wakuzisambaza huko majuu unashughulikiwa
Asalaam waaleykum

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment