Uzinduzi wa Five Star Modern Taarab "watoto wa bongo" Msasani club palikuwa hapatoshi!!

Bibie JOHA KASSIM kwa raha zake mdau aliendelea kudatisha mashabiki kitu kilichowafanya kushindwa kukalia viti vyao kama ulivyoona katika baadhi ya picha zao kundi hilo la Five Star Molden Taarab leo linaendelea na shoo kabambe pale kwenye ukumbi wa Equator Grill Mrtoni kwa Azizi Ally jioni ya leo
Kutoka kushoto ni HUSNA MAPUNDA, HUSNA KASIMU, ZENA MOHAMED,MARIAM HAMIS NA JOHA KASIM WAKIIMBA WAKATI WA UZINDUZI wakiwakilisha vilivyo kundi lao jipya kwa kweli walifanya mambo makubwa pale Msasani Club.

Huu ni zaidi ya Mzuka yaani ni shangwe kwa kwenda mbele, huyu hata akiamrishwa na mmoja wa waimbaji apande juu ya mti atapanda tu kwa raha zake babu we
Mashabiki wa kundi jipya la Five Star Molden Taarab wakishangweka kwa shangwe zisizokifani wakati wa uzinduzi wa kundi hilo uliofanyika usiku wa kuamkiia leo kwenye ukumbi wa Msasani Club jijini.




You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment