Katibu mkuu wa Wizara ya Afya Blandina Nyoni akiongea na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mh. Mwanaidi Maajar katika moja ya shughuli zake za kitaifa.
Na Anna Nkinda – Maelezo
04/07/2009 Serikali imesaini muendelezo wa makubaliano ya miaka minne ijayo na Mfuko wa Maendeleo Endelevu wa Novartis AG wa Switzerland kwa ajili ya kutoa dawa za kuzuia ugonjwa wa kifua kikuu nchini.
Makubaliano hayo ambayo ni ya kuanzia mwaka 2009 hadi 2012 yalifanyika leo Ikulu jijini Dar es Salaam kati ya Katibu Mkuu wa wizara ya Afya Blandina Nyoni na Mwenyekiti Mtendaji Mkuu wa Novartis AG Daniel Vasella na kushuhudiwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Katika makubaliano hayo Mfuko wa Novartis AG watatoa dawa za kuzuia ugonjwa wa kifua kikuu kwa wagonjwa wapya 250,000 kupitia Mfuko wa Dunia wa Kuhudumia Dawa (The Global Drug Facility - GDF) wa Shirika la Afya Duniani.
Mfuko wa Novartis AG unafanya kazi mbalimbali za afya hapa nchini tangu mwaka 1957 chini ya mwanzilishi wake Profesa Rudolf Geigy ambao ndio waanzilishi wa kituo cha utafiti wa maralia kilichopo Ifakara mjini Morogoro.
Aidha mfuko huo pia umekuwa ikitoa dawa kwa gharama naafuu chini ya Mpango wa Accredited Drug Dispensing Outlets (ADDO) ambao unaimarisha usawa wa upatikanaji wa dawa za maralia hapa nchini. Pia ni wasambazaji wa dawa mseto za maralia za ALU na kwa mwaka 2008 walitoa dozi 15.8 milioni.
Serikali yasaini mpango wa upatikanaji wa dawa za kuzuia ugonjwa wa kifua kikuu nchini!!
Posted by
ADMIN
You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment