Kundi la vijana wapatao 50 kutoka Tanzania watembelea “ Forbidden City ”nchini China!!.

Mfanyakazi wa kituo cha makumbusho cha Beijing ( Beijing Planning Exhibition hall) Bi. Cindy Wang akitoa ufafanuzi kwa kundi la vijana kutoka Tanzania kuhusu historia ya kale ya mji wa Beijing.Takribani vijana wapatao 50 wako nchini China kwenye ziara ya mafunzo kufuatia mwaliko wa rais wa nchi hiyo Hu Ji ntao alioutoa kwa rais wa Tanzania Jakaya Kikwete Februari mwaka huu.
Vijana kutoka Tanzania Bw. wakiongozwa na ofisa mipango wa Idara ya Kimataifa ya Chama cha vijana nchini China Ding Jiaming wakijiandaa kuingia katika eneo linalojulikana kama Forbidden City ambalo zamani lilitumika kama makazi ya wafalme nchini China . Eneo hilo llikuwa maalum kwa ajili ya makazi ya wafalme na familia zao tu na hakuruhusiwa mtu yeyote kuingia katika eneo hilo lakini kwa sasa baada ya kumalizika kwa utawala wa kifalme linatumika kama makumbusho ambapo watu wengi hufika a kujionea ufundi mkubwa uliotumika katika ujenzi wa makao hayo ya kifalme.

Hili ni eneo la mbele yalipokuwa makazi ya kifalme nchini China . Hapa wanaonekana wenyeji na wageni mbalimbali wakimiminika kwa wingi kutembelea eneo la makumbusho linalojulkana kama Forbidden City ambalo enzi za utawala wa kifalme haikuruhusiwa kwa mtu yeyote kuingia. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment