HAWA NDIYO WALIOVAA UHUSIKA KWENYE ONYESHO LA VIPAJI LA REDDS MISS ILALA JANA!!

Huyu aliyakata mauno kwa kwenda mbele katika muziki wa Taarab yaani ilikuwa si mchezo mpaka nilihisi labda ni Five Star Molden Taarab wanafanya mambo yao makubwa hii ilikuwa katika onyesho la vipaji la Redds Miss Ilala 2009 lililofanyika kwenye Hoteli ya Lamada Ilala ambapo warembo 17 walipanda jukwaani kuonyesha vipaji vyao katika nyanja mbalimbali ikiwa ni kuimba muziki, kucheza, kuigiza, ubunifu kuigiza na kadhalika
Redds Miss Ilala linatarajiwa kufanyika Agosti 7 kwenye viwanja vya ukumbi wa Karimjee jijini Dar es alaam Warembo wanaoshiriki kwenye shindano hilo ni Fatma Bongi, Everline Gamasa, Julieth Lugembe, Magreth Motau, Lilian Nyamizi Mihayo, Irene Karugaba, Neema Doreen Kasunga, Winnfrida Mmari, Husna Ahmed Doris Luis, Groly Mwandani, Pendo Lema, Anne Mkandawile, Khadija Mhecha, Sylivia Shally, Gladness Shao na Zena Mbasha pamoja na mwalimu wao Regina Joseph na matron Nelly Kamwelu aliyekuwa Miss Ilala namba mbili mwaka jana. .
Huyu aliigiza kama mbunifu wa mitindo kama unavyoona akifuma kitambaa mbele ya majaji.

Hapa ameshajifungua mtoto kama unavyomuona akimbebeleza.

Huyu kipaji chake kilikuwa kuigiza ambapo aliigiza kama mama mjamzito aliyekuwa shambani kisha akapatwa na uchungu na kujifungua mtoto hukohuko shambani.
Huyu aliimba nyimbo za kuabudu mpaka mishipa ikamtoka na aliigiza kwa hisia.

Majaji wakifuatilia kwa makini wakati wa onyesho hilo.

Wakuu wa Kamati ya Miss Tanzania wakiwa tayari katika onyesho la vipaji la Redds Miss Ilala ili kujua kinachoendelea kuanzia kushoto ni mwenyekiti wa kamati hiyo Prashant Patel, Mh. Yakub aliyekuwa Naibu meya wa Manispaa ya Ilala Mkurugenzi Miss Tanzania Hashim Lundenga,Mkuu wa Itifaki Albert Makoye na Mkuu wa Uhusiano Yason Mashaka.

Mbunifu wa mavazi Asia Idarous katikati akiwa katika pozi na warembo mablimbali waliojitokeza katika onyesho hilo lililofanyika kwenye Hoteli ya Lamada jana.

mashabiki mbalimbali waliojitokeza katika onyesho la vipaji la Redds Miss Ilala 2009 lililofanyika katika Hoteli ya Lamada Ilala.
keza ka

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

1 comments:

  1. Mhh!

Post a Comment