WATAALAMU WAZUNGUMZIA UTATUZI WA MIGOGORO AFRIKA.

Mkurugenzi wa Taasisi ya amani na utatuzi wa migogoro barani Afrika (IPCS) Cosmas Bahali akifungua mafunzo ya kutunza amani barani Afrika (jana) katika ukumbi wa mikutano hoteli ya Beach Komba jijini Dar es Salaam.Washiriki kutoka nchi 19 barani Afrika wanashiriki mafunzo hayo yaliyofadhiriwa na serikali ya Norway.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya kutunza amani barani Afrika wakifuatilia mafunzo yaliyoandaliwa na Taasisi ya amani na utatuzi wa migogoro barani Afrika (IPCS) yanayoendelea katika ukumbi wa mikutano katika hoteli ya Beach Komba jijini Dar es Salaam.

Washiriki wa mafunzo ya kutunza amani kutoka katika nchi 19 barani Afrika wakiwa katika picha ya pamoja nje ya ukumbi wa mikutano wa hotel ya Beach Komba jijini Dar es Salaam.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment