Ofisa Mtendaji mkuu wa Tamasha la nchi za Jahazi ZIFF Prof. Martin Mhando akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano uliofanyika katika kituo cha utamaduni cha Ufaransa Alliance Francaise juu ya maandalizi ya tamasha hilo, linalotarajiwa kuanza juni 24 mpaka julai 4 mjini Zanzibar likishirikisha wanamuziki na wasanii kutoka nchi mbalimbali, ambapo kutakuwa na maonyesho mbalimbali ukiwemo muziki, Filamu, semina mbalimbali juu ya mapambano ya Ukimwi, Ngoma za Asili na mambo mengine mengi, huku mgeni rasmi wa Tamasha hilo akiwa mwigizaji filamu maarufu kutoka Hollwood nchini Marekani anayejulikana kama Danny Glover, wengine katika picha ni Hassan Mitawi katikati mwenyekiti wa ZIFF na mwisho kushoto ni Murugenzi wa kituo cha utamaduni cha Ufaransa Alliance Francaise Didier Martin.
Mwandishi wa habari kutoka shirika la utangazaji Tanzania TBC Evance Mhando aliyeshika kipaza sauti akiuliza swali wakati wa mkutano na waandaaji wa Tamasha la nchi za Jahazi ZIFF katika mkutano na wanahabari uliofanyika kwenye kituo cha utamaduni cha ufaransa Alliance Francaise leo.
Mwanamuziki Mwasiti kutoka THT akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano huo juu ya ushiriki wake katika tamasha la nchi za Jahazi ZIFF.
Mtangazajiwa Star Televisheni Saida Mwilima akimhoji msanii Kassim Mganga aliyeimba wimbo wa (Anewa) ambaye ni miongoni mwa wasanii watakaofanya onyesho katika Tamasha la nchi za jahazi ZIFF linalotarajiwa kuanza Juni 27 mpaka julai 4 mwaka huu mjini Zanzibar kulia ni mwandishi wa Star Televisheni Agness Baharia.
1 comments:
njoo unihoji geto uone
Post a Comment