Makamu wa Rais Dk Ally Muhamed Shein akiongea na Balozi wa Japan nchini Hiroshi Nagawa wakati alipomtembelea kwa mazungumzo ofisini kwake leo.
Clarence Nanyaro, Ofisi ya Makamu wa Rais
Serikali ya Japan itatoa shilingi bilioni 14,216,000,000 kugharamia mradi wa maji safi na salama kwa mikoa ya Mwanza na Mara ambao utatekelezwa kwa awamu tatu kuanzia septemba 2009 hadi 2011.
Akizungumza na Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein Jijini Dar es salaam leo, Balozi wa Japan hapa nchini Hiroshi Nagawa amesema kuwa serikali ya Japan inafurahishwa na mipango ya serikali ya Tanzania kuwapatia wananchi huduma za kijamii na nchi hiyo itaendelea kutoa misaada na kuimarisha ushirikiano uliopo.
Mradi huo wa maji safi na salama ambao utatekelzwa katika mikoa hiyo unategemewa kunufaisha vijiji 44 na kuongeza idadi ya watu watakaopata maji safi na salama kutoka 9,400 hadi 55,000.
Balozi Nagawa amesema kuwa kuwa samabamba na kugharamia mradi huo,pia serikali ya Japan itakamilisha ujenzi wa barabara ya Kilwa na kufanya upanuzi wa barabra hiyo hadi katika ya jiji la Dar Es salaam.
Balaozi Nagawa ameongeza kuwa,ili kuimarisha hali ya usafiri jiji Dar Es salaam, Japan itafanya upanuzi wa barabara ya Bagamoyo kuanzi eneo la Moroco hadi Tegeta kati ya Julai na Desemba mwaka huu.
Serikali ya Japan pia inafadhili ujenzi wa barabra ya kutoka Arusha kupitia Namnaga hadi Athi nchini Kenya.
Sambamba na balozi wa Japan,Dk Shein pia alionana na Mabalozi wa Denmark na Misri hapa nchini. Akizungumza na Makamu wa Rais, Balozi wa Denmark Bjarne Sorensen ambaye aliwasilisha ripoti ya kamisheni ya Afrika kuhusu kuongeza ajira kwa vijana ,aliitaka serikali kuendelea kuzifanyia barabara matengenezo badala ya kuziacha zikachakaa na kujenga upya ili kupunguza gharama.
Serikali ya Denmark ndiyo inagharamia upanuzi wa barabara kutoka Chalinze hadi Segera ambapo itakapo kamilika itakuwa na uwezo wa kupitisha magari mawili upande mmoja.Uzinduzi wa upanuzi wa barabara hiyo ulifanyika mwezi Mei mwaka huu katika eneo la Lugoba.
Aidha ,kuhusiana na ripoti ya kamisheni ya Afrika balozi Sorensen amesema kwa sasa wanandaa jinsi ya kuinadi ripoti hiyo katika Taasisi za kimataifa ili iwe ajenda ya kudumu na kuweza kuondoa tatizo la ajira linalowakabili Vijana wengi kwa sasa. Mkutano wa Kujadili matatizo ya ajira kwa vijana ulifanyika mwezi machi mwaka huu nchini Tanzania.
Kwa upande wake, balozi Wael Adel Nasr wa Misri, amesema kuwa kuanza tene kwa safari za shirika la ndege la Misri kutainifaisha Tanzania kutokana na kuleta watalii wengi.
Pia Misri imefuangua ofisi za kanda za shirika lake la ndege hapa Tanzania ili waweze kuhudumia wasafiri kutoka katika nchi nyingi zinzoizunguka Tanzania.
Serikali ya Misri pia inafadhili uchimbaji wa visima 30 katika Wilaya ya Same kwa lengo la kuwapatia wanachi maji na mradi huo unatagemea kuzinduliwa mwezi ujao mwanzoni.

0 comments:
Post a Comment