DAR SLAAM POETRY 2009 KUFANYIKA MWEZI UJAO!!

Habari njema kutoka kwa Mrisho Mpoto katikati kwenye picha ni kwamba amepewa leseni ya kuendesha mashindano hayo hapa nchini ambayo yataitwa (Dar Slaam Poetry 2009) baada ya kuonyesha uwezo wake katika nyanja hiyo inayopendwa sana katika mabara ya Ulaya na Amerika, Mrisho amesema kwa kuanza watatafuta wawakilishi wa mwaka huu kwa mkoa wa Dar es alaam tu kutokana na muda wa maandalizi kuwa mfupi sana ambapo watatafutwa wawakilishi wawili watakaowakilisha nchi kwenye shindano lijalo litakalofanyika katika Visiwa vya ReUnion Ufaransa yanayotarajiwa kufanyika mwezi Septemba tarehe 28 hivyo waandaaji wa mashindano hayo kwa Wilaya za Kinondoni na Temeke tayari wamehapatikana na majina yao ni Amani Kipimo Temeke aliyeko kushoto katika picha na huku kinondoni akiwa Simon Mwakifwamba aliyeko kulia katika picha na mchakato wa kumtafuta mwandaaji wa wilya ya Ilala bado unaendelea, ambapokatika kujiweka sawa tayari mikakakati imeanza na kikao cha kwanza kimefanyika leo kwenye ukumbi wa Sanaa Pub FULLSHANGWE inakutakia kila mafanikio Mjomba Mpoto na kamati yako ili kuendeleza juhudi zako ulizozionyesha huko Ufaransa.

Mrisho Mpoto kushoto akiwa na mshindi wa shindano hilo wa dunia Joachim ambaye ni Mmarekani akiwa na Tuzo yake, mara baada ya kumtangaza mshindi katika shindano hilo ,jumla ya nchi 16 zilishiriki katika shindano hilo ambalo hufanyika kila mwaka nchni Ufaransa ambapo Mpoto aliibuka na kushika nafasi ya Tatu kitu ambachi kianmuweka kwenye ramani nzuri ya washairi wazuri Duniani.
Hapa mpoto akiwa na washabiki wake mbaimbali mara baada ya shindano hilo.

Hapa Mjomba Mpoto akiwafundisha wanafunzi darasani katika moja ya shule alizotembelea akiwa nchini Ufaransa kwa ajili ya shindano la World Slaam Poerty la dunia lililofanyika nchini humo na kuibuka mtu wa tatu.
Mjomba akiwafundisha baadhi ya wakazi wa jiji la Paris tungo za mashairi ya kiswahili kwakweli mjomba amefanikiwa kwa kiwango kkubwa kutangaza Tanzania na utamaduni wa Lugha yake ya Kiswahili.

Mrisho mpoto Mjomba akiwa katika mitaa ya Jiji n la Paris pamoja na washiriki wengine wa shindano hilo lililofanyika hivi karibuni jijini humo nchini Ufaransa Mjomba Mpoto alishika. nafasi ya tatu

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

1 comments:

  1. mpoto uko juu kaka. kaza buti...

Post a Comment