Usiku wa Mwafrika, Kuala Lumpur-Malaysia Wafana!!

Si mchezo kusimama hapo ninaimani hata Obama alianzia chini kama hivi ipo siku!! Mdau Pius wa Spoti na Starehe Blog akizungumza kwenye sherehe hizo.
Kwa mara nyingine tena Jumuiya ya Mabalozi toka Africa walioko Malaysia wamefanikisha ile siku ya African Day katika Hotel ya Marriott hapa Kuala Lumpur Malaysia iliyofanyika jana, ni siku ambayo inakutanisha waafrika walioko Malaysia na kusherehekea na kubadilishana mawazo. Balozi wa Tanzania hapa Malaysia Mh. Abdul Sisco Mtiro hakuhudhuria sherehe hizo kwani yuko nchini Cambodia alikokwenda kuwakilisha hati zake za utambulisho wa Ubalozi kwani Mh. Sisco anawakilisha Malaysia, Singapore, Cambodia, Laos, Philipines na Indonesia, Kulikuwa na maonyesho ya vitu tofauti tofauti kutoka mataifa tofauti na nchi mbali mbali zilikuwa na meza zao ambapo walitambulisha nchi zao ama kwa utamaduni au kwa vivutio vya aina mbali mbali ukiwemo Utalii, Sherehe hizi huwa zinaandaliwa kwa pamoja na mtandao wa Mabalozi wa Afrika waliko Malaysia na kugharamiwa na mtandao huo pia bila kiingilio kwa kinywaji au kilaji, ambapo waafrika hukutana na chakula toka kila pembe ya Afrika huwepo pia.

Maneno yaliyotengenezwa maalum kwa ajili ya hafla hiyo kama yanavyoonekana yakisomeka AFRICA

Watanzania Yusra toka Zanzibar na Salim wakipiga picha ya kumbukumbu kwenye> usiku huo ambao hufanyika mara moja kwa mwaka

Yusra, Noel na Iyah wakiwakilisha Tanzania.

Mdau Pius akiwa na Balozi wa Swaziland Malaysia akiwa na mkewe na mwanaye kwenye sherehe hiyo.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment