ONYESHO LA KHANGA ZA KALE LAFANA DIAMOND!!

Na hapa mwanamke akinyonyesha mtoto wake hii yote ilikuwa jana pale Diamond Jubilee katika onyesho la Khanga za Kale ililoandaliwa na Fabac Fashion, chini ya Mwnamitindo Asia Idarous ikishirikisha wabunifu wengine kama Francwaa, Zamda George, Paka Wear, Farha na wengine, burudani zikitolewa na Spice Molden Taarab kutoka Zanzibar na Kalunde Band ya Deo Mwanambilimbi, kwa mtukio zaidi ya onyesho hilo shuka chini mdau upate uhondo wa onyesho hlio.
Hapa akijifukizia Udi.
Mwnamke akipika avaeje khanga hebu picha hii cheki mdau.





Mwenyekiti wa UWT Mama Sophia Simba kati aliyekuwa mgeni rasmi akisoma hotuba yake wakati wa onyesho hilo kulia ni Idarous Khamsini na Kushoto ni mbunifu Asia Idarous Khamsini ambaye ndiye aliyandaa onyesho hilo lililojulikana kama Khanga za Kale.
Kalunde Band wakitumbuiza katika onyesho hilo huku wakiwa wamejipigilia vivazi vilivyotengenezwa kwa Khanga.

Manka Mush mwandaaji wa Miss Highlearning akiwa amejipigilia kivazi chake huku akiwa ametulia tuli na kilongalonga chake.

Wabunifu Francwaa kulia na Zamda George wakila pozi mbele ya Camera ya FULLSHANGWE.

Zain nao na khanga zao hawataki kubaki nyuma hebu cheki hawa vimwana wao walivyotinga viwalo mdau.

Nasreem Karim Miss Tanzania 2008 kulia na Mwanamitindo Flaviana Matata hawakuwa nyuma kushuhudia onyesho hilo.

Hizi na baadhi ya nguo na bidhaa mbalimbali zilizoonyeshwa katika Onyesho hilo hizi ni nguo zinazotebuniwa na Belinda Mlingo.
Kuazia kulia ni Babu Njenje, Kanumba, Ray na Richard wakiwa katika ukumbi wa Diamaond Jubilee kujionea kilichokuwa kikiendelea katika onyesho jlio.

Mercy Galabawa wa pili kutoka kulia na Pita Mwendapole wa New Habari Cooperationa wakiwa na marafiki zao katika onyesho hilo

Mmoja wa wafanyabiashaera walioonyesha mavazi yao akipambwa kwa michoro mbalimbali katika ukumbi huo huyu anaitwa Belinda Mlingo.

Watu mbalimbali wakliohudhuria onyesho hilo katika ukumbi wa Diamaond Jubilee wakifuatilia kwa karibu onyesho hilo jana.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment