
Haya sasa huyu ndiyo Beatrice Lukindo Miss Vodacom IFM 2009, Kimwana atakayewakilisha chuo hicho katika mashindano ya kanda ya Vyuo vikuu yatakayofanyika mwezi juni, mlimbwende huyu amepatikana katika shindani lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Msasani Club jijini Dar na kuibuka na kitita cha shilingi laki 500.000 taslimu na zawadi zingine kutoka maduka ya nguo ya KP Mdau pata matukio mbalimabli katika picha juu ya yaliyojiri katika shindano hilo lililokuwa zuri tulivu na la kuvutia.

Miss Vodacom IFM Beatrice Lukindo akiwa pamoja na washindi wenzake, wakipozi kwa picha na mwandaaji wa Miss Highlearning na aliyekuwa jaji mkuu wa shindano hilo Manka Mushi kushoto na kulia ni George Rwehumbiza Meneja Udhamini na Mawasiliano wa Vodacom ambao ndiyo wadhamini wakuu wa Miss Vodacom Tanzania.

Hapa washindi wa Miss Vodacom IFM wakiwa katika picha ya pamoja na majaji wa shindano hilo mara baada ya kutangazwa washindi wa shindano hilo usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Msasani Club.

Miss Vodacom IFM Beatrice Lukindo akiwapungia mkono mashabiki wake mara baada ya kuibuka kidedea katika shindano la kumtafuta mrembo atakayewakilisha chuo cha IFM katika shindano la Miss Vodacom Highlearning linalotarajiwa kufanyika mwezi ujao kushoto ni mshindi wa pili Esther Gao na kushoto ni mshindi wa tatu Veronica Micky.

Hapa wakiulizwa maswali tayari kwa kuwapata washindi wa Miss Vodacom IFM na kulia ni Jaji mkuu Manka Mushi akiwasomea maswali warembo hao.

baada ya kupita na vazi la jioni hawa ndiyo warembo walioingia Top Five ya Miss Vodacom IFM kutoka kushoto ni Beatrice Lukindo, Esther Gao, Veronica Nicky,Annet Brayson na Francisca Mansilo.

0 comments:
Post a Comment