(Na Martina Nkurlu)
Ili kukuza vipaji vya vijana Vodacom Tanzania hivi karibuni imekipiga jeki Chama cha Mchezo wa Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) kwa kulipia gharama za Ushuru wa Forodha wa mipira 210 iliyoingizwa nchini kama msaada kutoka Shirikisho la Mchezo huo Afrika (FIBA AFRICA) .
Mipira itatumika katika kutekeleza programu yenye lengo la kufanikisha mpango maalum wa kuvumbua na kuendeleza vipaji vya vijana walioko shule za msingi na sekondari katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Mkuu wa Kitengo cha Udhamini na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, George Rwehumbiza, anasema Vodacom imetoa ushirikiano huo ikiwa ni sehemu ya mikakati yake ya kuendeleza michezo hapa nchini.
Rwehumbiza amesema kila mara kampuni yake imekuwa ikidhamini michezo mbalimbali ambayo mbali na kutengeneza ajira pia imekuwa ikiwasaidia vijana kuepukana na matatizo ya kijamii kama vile uvutaji wa bangi, ulevi, matendo yanayoweza kuwaharibia maisha yao ya baadaye na kuwaletea maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi.
“Tutaendelea kushirikiana na serikali katika kuhakikisha kwamba michezo inakua na kuitangaza nchi yetu katika jukwaa la kimataifa,”
“Ndiyo maana tunawekeza katika sekta ya michezo kwani mbali na faida nyingine tunajua umuhimu wa michezo katika kuitangaza nchi yetu,
”Naye Katibu Mkuu wa TBF, Lawrence Cheyo anaishukuru Vodacom Tanzania kwa kutoa shilingi milioni moja kulipia ushuru wa mipira hiyo.
Amesema mipira hiyo imeletwa nchini ikiwa ni sehemu ya mpango wa TBF na FIBA AFRICA kukuza mchezo huo kwa vijana wa Shule za Msingi na Sekondari hapa nchini.
“Kwa niaba ya TBF ninatoa shukrani zangu za dhati kwa Vodacom kwani mmeonyesha jitihada zenu za kukuza michezo hapa nchini,” anasema
Anafafanua kwamba mipira hiyo imetolewa na FIBA AFRICA yenye makao makuu yake nchini Ivory Coast.

0 comments:
Post a Comment