SHINDANO LA MALTA GUINESS STREET DANCE AFRICA LAZINDULIWA!!

Kikundi cha Bombeso kikitumbuiza wakati wa uzinduzi wa shindano hilo Helenic Club.


Malta Guiness kinywaji kisicho na kilevi imezindua Dansi la wachezaji dansi wa mitaani yaani Malta Uginess Street Dance Afrika, shindano hili la kusisimua litafanyika ili kumpata mcheza dansi mahiri na mwenye kipaji ambapo watashindanishwa vijana mbalimbali hapa nchini ili kumpata mshindi atakayewakilisha nchi.
Mashindano haya kwa ajili ya kumpata bingwa wa Dunia itakuwa ni mara ya kwanza kufanyika katika jiji la Nairobi nchini Kenya mwezi agosti mwaka huu na hii itakuwa ni mara ya kwanza kufanyika barani afrika na ukanda wa Afrika Mashariki.
Wacheza Dansi kutoka Tanzania watashindanishwa na mabingwa wenzao wa kitaifa kutoka bara la Afrika, Ulaya Amerika na Asia katika fainali itakayofanyika Agosti 2009.


Nchi zingine za Afrika zitakazotoa wawakilishi katika mashindano hayo ni Cameroun, Ghana, Nigeria na Kenya
Kwa hapa nyumbani tratiba ya mashindano hayo itakuwa kama ifuatavyo tarehe 9/5/2009 usaili utafanyika Morogoro Mt Uruguru, 23/5/2009 Mwanza Villa Park, 6/6/2009 Tanga Tanga Hotel, 20/6/2009 Zanzibar Ngome Kongwe, 4/7/2009 Arusha Matongee Club, 19/7/2009 Dar es alaam Coco Beach 1/8/2009 itakuwa fainali jijini Dar es alaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment