Mwanzilishi na mkurugenzi wa chama cha madaktari waafrika nchini Marekani Ted Alyemayhu akimkaribisha Mwenyekiti wa Taasisi ya wanawake na Maendeleo (WAMA) mama Salma Kikwete kwa kumpatia maua wakati alipowasili katika mkutano wa wake wa marais wa Afrika uliojadili juu ya Afya jijini Los Angeles Marekani.
Los Angles, Carfonia 24/04/2009 Watanzania wanaoishi nje ya nchi wametakiwa kudumisha utamaduni wao ikiwa ni pamoja na kuongea lugha ya Kiswahili pasipo kuogopa kwani ndiyo utambulisho wa taifa lao .
Hayo yamesemwa jana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) wakati akiongea na watanzania waishio mjini Los Angles, Carfonia.
“Hivi sasa lugha ya kiswahili ni rasmi na inatambulika katika Umoja wa Mataifa kazi mliyokuwa nayo ni kukienzi Kiswahili kwa kuongea Kiswahili fasaha kwani pale mtu atakapokusikia unaongea lugha ya Kiswahili atafahamu kuwa wewe ni mtanzania”, alisema mama Kikwete.
Aliendelea kusema kuwa hakuna taifa lisilokuwa na utamaduini wake na hakuna lugha iliyo bora zaidi ya nyingine kwani hivi sasa wamarekani weusi ambao asili yao ni Afrika wanahangaika asili ya nchi zao kabla ya mababu zao kuchukuliwa utumwa na kuletwa Marekani.
Aidha Mama Kikwete aliwashauri watanzania hao kukumbuka nyumbani walikotoka kwa kuwapelekea ndugu zao misaada mbalimbali zikiwemo fedha ambazo watazitumia katika kupambana na hali ngumu ya maisha kuliko kuishi maisha ya juu wakati ndugu zao wanateseka.
Mama Kikwete alisema, “Kutokufika nyumbani siku nyingi si sababu ya kutokujua hali ya nyumbani kwenu ikoje kwani kuna balozi wetu hapa Marekani ambaye anaweza kuwapa taarifa au muingie katika mtandao mbalimbali na kujua hali halisi ya nchi yenu”.
“Serikali inajukumu la kujenga shule, barabara, hospitali na miundo mbinu mingine lakini jukumu la kujenga nyumba ya kuishi ni lako wewe mwenyewe hivyo kama hutajitahidi kujenga nyumbani kwenu siku utakayopata matatizo sijui utakimbilia wapi ndugu yangu?”, aliuliza.
Mama Kikwete pia aliwataka watanzania hao kufuata taratibu na sheria za nchi husika na kutojiingiza katika biashara zisizofaa ikiwemo ya madawa ya kulevya kwa kudhani kuwa serikali itawasaidia .
Mwenyekiti huyo wa WAMA alisema, “Mmetoka nyumbani na kuja kufanya kazi, biashara au kusoma katika nchi ya watu basi waliokuja kusoma wahakikishe kuwa wanatimiza lengo walilokusudia na kurudi nyumbani pale watakapomaliza masomo na si kungángánia ugenini kwani nyumbani ni nyumbani”.
Na Anna Nkinda – Maelezo

0 comments:
Post a Comment