MASHINDANO YA MISS EAST AFRIKA 2009 YAZINDULIWA BUJUMBURA!!

Muandaaji wa Miss East Afrika kulia na Bw. Lena Calist na na Miss East Afrika wakiwa Mjini Bujumbura hivi karibuni
MISS EAST AFRICA 2009
02/02/2009

* MASHINDANO YA MISS EAST AFRICA 2009 YAMEZINDULIWA RASMI JANA TAREHE 31/01/2009 JIJINI BUJUMBURA NA KUHUDHULIWA NA WATU MBALIMBALI MASHUHURI AKIWEMO RAIS MSTAAFU WA NCHI HIYO NDUGU PIERRE BUYOYA.

* AKITANGAZA RASMI TAREHE YA KUFANYIKA KWA MASHINDANO HAYO, MKURUGENZI WA RENA EVENTS LIMITED YA JIJINI DAR ES SALAAM AMBAO NDIO WAANDAAJI WA MASHINDANO HAYO, NDUGU RENA CALLIST, ALISEMA KWAMBA FAINALI ZA MASHINDANO YA MISS EAST AFRICA MWAKA HUU ZITAFANYIKA SIKU YA IJUMAA TAREHE 07/08/2009 JIJINI BUJUMBURA BURUNDI KUANZIA SAA 1:35 USIKU KWA SAA ZA BURUNDI (SAWA NA SAA 2:35 USIKU KWA SAA ZA TANZANIA.)

* HII ITAKUWA NI MARA YA PILI MFURULIZO KWA MASHINDANO HAYO KUFANYIKA NCHINI BURUNDI KUFUATIA MASHINDANO HAYO KUFANYIKA NCHINI HUMO MWISHONI MWA MWAKA JANA KWA MAFANIKIO MAKUBWA.

* MASHINDANO HAYO YANAFANYIKA TENA NCHINI HUMO KUFUATIA
OMBI LA RAIS WA BURUNDI NDUGU PIERRE NKURUNZIZA ALIYEMUOMBA MKURUGENZI WA RENA EVENTS NDUGU RENA CALLIST AKITAKA MASHINDANO HAYO YAFANYIKE TENA NCHINI BURUNDI BAADA YA KURIDHISHWA NA KIWANGO CHA HALI YA JUU CHA MASHINDANO YALIYOFANYIKA MWAKA JANA NCHINI HUMO AMBAPO YALIWEZA KUITANGAZA SANA NCHI YA BURUNDI HUSUSAN KATIKA NYANJA ZA KITAMADUNI NA KI UTALII.

* KATIKA MASHINDANO YA MWAKA JANA MREMBO CLAUDIA NIYONZIMA WA BURUNDI ALIIBUKA MSHINDI WA MASHINDANO HAYO NA KUJINYAKULIA GARI LA KISASA AINA YA LEXUS RX 300 LENYE THAMANI YA TSHS MILLIONI 35. MASHINDANO HAYO YALITIZAMWA “LIVE”NA WATU WANAOKADIRIWA KUFIKIA MILLIONO 200 DUNIANI KOTE KUPITIA NJIA YA INTERNET NA VITUO MBALIMBALI VYA TELEVISION AMBAPO YALIWEZA KUONYESHA SURA MPYA YA BURUNDI YENYE MATUMAINI MAKUBWA YA MAENDELEO YA KIUCHUMI BAADA YA KUMALIZIKA KWA VITA VILIVYODUMU KWA MUDA MREFU NCHINI HUMO.

* KATIKA UZINDUZI HUO RAIS PIERRE NKURUNZIZA ALISEMA
SERIKALI YAKE ITAMSAIDIA MREMBO CLAUDIA NIYONZIMA KATIKA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE KATIKA JAMII HASWA KATIKA KUSAIDIA WATOTO YATIMA; KATIKA HOTUBA YAKE ILIYOSOMWA KWA NIABA YAKE NA WAZIRI WA MASUALA YA AFRIKA MASHARIKI, MHESHIMIWA HAFSA MOSI,RAIS PIERRE NKURUNZIZA PIA ALIZIOMBA SERIKALI ZA NCHI WASHIRIKI KUMSAIDIA MREMBO HUYO KWA KUWA YEYE SASA NI BALOZI WA UTAMADUNI NA AMANI WA AFRIKA MASHARIKI. RAIS PIERRE NKURUNZIZA PIA ALISEMA KATIKA HOTUBA YAKE KWAMBA SERIKALI YAKE IWASAIDIA IPASAVYO WAANDAAJI WA MASHINDANO HAYO ILI KUHAKIKISHA KWAMBA YANAFANIKIWA KWA KUWA WAANDAAJI HAO WAMEAMUA KUCHAGUA TENA NCHI YAKE KUWA MWENYEJI WA MASHINDANO YA MISS EAST AFRICA 2009 NA KWAMBA HIYO NI HESHIMA KUBWA KWA NCHI YA BURUNDI

* NAYE RAIS MSTAAFU WA BURUNDI NDUGU PIERRE BUYOYA ALIIPONGEZA KAMPUNI YA RENA EVENTS LIMITED KWA KUENDESHA MASHINDANO YA MWAKA JANA KWA MAFANIKIO MAKUBWA NA KUMSHUKURU NDUGU RENA CALLIST NA KAMPUNI YAKE KWA KUAMUA KUFANYA TENA MASHINDANO HAYO NCHINI BURUNDI

* MASHINDANO YA MISS EAST AFRIKA MWAKA HUU YATAZISHIRIKISHA NCHI 14 ZA UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI AMBAZO NI TANZANIA, BURUNDI, RWANDA, KENYA NA UGANDA. ZINGINE NI DJIBOUTI, ERITREA, ETHIOPIA, SOMALIA, PAMOJA NA VISIWA VYA MAURITIUS, COMOROS, RE UNION, MADAGASCAR NA SEYCHELLES.

* MISS EAST AFRICA KWA SASA NDIO MASHINDANO MAKUBWA YA UREMBO KATIKA UKANDA HUU WA BARA LA AFRIKA NA MWAKA HUU YANATARAJIWA KUTIZAMWA NA MAMILIONI YA WATU WENGI ZAIDI DUNIANI KUPITIA VITUO MBALIMBALI VYA TELEVISION NA INTERNET AMBAPO PAMOJA NA MAMBO MENGINE, MASHINDANO HAYO YANAKUSUDIA KUTANGAZA UTAMADUNI WA WATU WA AFRIKA MASHARIKI PAMOJA NA KUONYESHAVITUO MBALIMBALI VYA UTALII VILIVYO KATIKA ENEO LA AFRIKA YA MASHARIKI.

* SHEREHE ZA UZINDUZI WA MISS EAST AFRICA 2009 ZILIFANA SANA KWA KUPAMBWA NA BURUDANI MBALIMBALI PAMOJA NA “FIREWORKS” ZA UMBARI WA KILOMETA TANO JUU ANGANI AMBAPO MBALI NA RAIS MSTAAFU NDUGU PIERRE BUYOYA PAMOJA NA WAZIRI WA MASUALA YA AFRIKA MASHARIKI, WENGINE WALIOHUDHURIA SHEREHE ZA UZINDUZI WA MISS EAST AFRICA 2009 NI PAMOJA NA MAWAZIRI MBALIMBALI WA SERIKALI YA BURUNDI, NA MABALOZI WA NCHI ZA NJE WALIOKO BURUNDI IKIWA NI PAMOJA NA BALOZI WA MAREKANI NCHINI HUMO NA WAGENI WENGINE WENGI MAARUFU.


BY: RENA CALLIST,
BUJUMBURA, BURUNDI TEL: +255 755 755 755

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment