Wahandisi (Engineer) wa Kampuni ya SEACOM Tanzania Limited wakiwa wanafunga kamba ili kuvuta waya (cable) kutoka ndani ya meli iliyotia nanga bahari ya Hindi ambao utawekwa katika kituo chao kilichopo Kunduchi Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutoa huduma hiyo Nchini takayoanza mwezi wa sita mwaka huu mara baada aya kukamilika kwa ujenzi wa kituo hicho.
Wafanyakazi ya Kampuni ya SEACOM Tanzania Limited wakiwa wamebeba waya ( fibre optic cable) kutoka ndani ya meli iliyotia nanga bahari ya Hindi ambao utawekwa katika kituo chao kilichopo Kunduchi Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutoa huduma ya mwasiliano Nchini. Kampuni hiyo itaanza kutoa huduma hiyoya mawasiliano Nchini mwezi wa sita mwaka huu mara baada aya kukamilika kwa ujenzi wa kituo hicho.Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa kampuni hiyo Michael Njumba akifuatiwa na Meneja Mkurugenzi Anna Rupia na kushoto ni Eng. Jon Avery.
Wafanyakazi ya Kampuni ya SEACOM Tanzania Limited wakiwa wamebeba waya ( fibre optic cable) kutoka ndani ya meli iliyotia nanga bahari ya Hindi ambao utawekwa katika kituo chao kilichopo Kunduchi Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutoa huduma ya mwasiliano Nchini. Kampuni hiyo itaanza kutoa huduma hiyoya mawasiliano Nchini mwezi wa sita mwaka huu mara baada aya kukamilika kwa ujenzi wa kituo hicho.Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa kampuni hiyo Michael Njumba akifuatiwa na Meneja Mkurugenzi Anna Rupia na kushoto ni Eng. Jon Avery.
Na Anna Nkinda – Maelezo
Kampuni ya SEACOM Tanzania Limited imeanza kujenga kituo cha waya (Cable) kwa ajili ya kutoa huduma ya waya wa mawasiliano itakayowawezesha wadau wa mawasiliano nchini kupata huduma hiyo kwa gharama naafuu. Huduma hiyo inatarajia kuanza mapema mwezi wa sita mwaka huu mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa kituo hicho kilichopo Kunduchi jijini Dar es Salaam. Meneja Mkurugenzi wa kampuni hiyo Anna Rupia ameyasema hayo leo wakati akiongea na waandishi wa habari waliofika katika kituo hicho kuona maendeleo ya ujenzi wa Cable hiyo ambayo itafungwa kutoka bahari ya Hindi na kuunganishwa na vituo vingine. “fibre optic Cable hii ya mawasiliano kwa upande wa Afrika itaanzia katika vituo vya Afrika ya Kusini, Maputo, Dar es Salaam, Mombasa na Djibout hivyo basi kituo cha Dar es Salaam kitaunganishwa na vituo hivi ”, alisema Rupia. Aliendelea kusema kuwa kwasasa makampuni ya mawasiliano yananunua satelite kwa kipande kimoja cha mega bites (1MBPS) kwa dola za Kimarekani 3000 wakati Kampuni hiyo itakapoanza kutoa huduma watapunguza bei na kuuza kwa dola za kimarekani 100. Baada ya kumaliza kazi ya kujenga kituo hicho watasambaza network nchi nzima kwa kupitia makampuni mbalimbali za simu ambayo yatasambaza hadi nchi za jirani ambako hakuna bahari kama Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda, Burundi, Zambia. Naye Mkurugenzi wa kampuni hiyo Michael Njumba alisema kuwa wateja wao watakuwa ni makampuni ya Simu na Internet hivyo basi pale watakapoanza kutoa huduma ni muhimu kwa wateja hao kupunguza bei kwa kuwa watakuwa wamepunguziwa bei ya kununu mega bites. Mkurugenzi huyo alisema, “tunategemea kuwa ifikapo mwaka 2010 watanzania wengi wataona mashindano ya kombe la Dunia kwa kupitia simu zao za mkononi kwani gharama za simu zitakuwa zimeshuka tofauti na ilivyo sasa”. Aidha Mhadhiri na Mkuu wa Idara ya Teknologia ya Uhandisi na Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dk. Leonard Chamuriho alisema kuwa chuo hicho kimepewa bure (STM 11) sawa na Mega Bites 155 (155MB) kwa ajili ya kufundishia wanafunzi. Kampuni hiyo inafikiria kutoa huduma kama hiyo kwa Chuo Kikuu cha Dodoma kwa siku za baadaye. Gharama ya Mradi mzima ambao umeanza mwaka 2006 kwa Afrika ya Mashariki na Kusini ni dola za kimarekani milioni 600 na nia ya mradi huo ni kupunguza gharama za mawasiliano Nchini. Mwisho.
0 comments:
Post a Comment