ZOOM,ZOOM,ZOOM YA MWANAMUZIKI SIZ AZIZI YAJA KAENI MKAO WA SHANGWE!!

Mzee wa Zoom, Zoom,Zoom Siz Azizi katika pozi la mauzo.

Wanamuziki wa kundi la B. Band kutoka kulia Siz Azizi, Banana Zorro. Ismail mmoja wanamuziki wa kundi hilo mbele ya Camera ya FULLSHANGWE.

Mwanamuziki wa Bendi ya B. Band ya jijini inayoongozwa na mwanamuziki machachari Banana Zorro Siz Azizi ameiambia Tovuti ya FULLSHANGWE kwamba yuko mbioni kuipua Single yake itakayokwenda kwa jina la Zoom Zoom Zoom hili ndilo jina aliloamua kuipa nyimbo yake hii anayoilelezea kuwa itakuwa ni ya mwaka mara itakapoanza kusikika masikioni mwa mashabiki na wapenzi wa muziki wa bongofleva.
Anasema kuwa Zoom Zoom ni mlio wa nyuki wakati anapokuwa mawindoni akitafuta malighafi katika maua mazuri li aweze kutengeneza asali, Siz anasema katika nyimbo hiyo ambayo amerekodi katika studio za Maneke studio zilizopo sinza mlio wa nyuki unamaanisha mapenzi ya hali ya juu kwa wapendanao na ameitunga nyimbo hii maalum kwa siku ya wapendanao inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 14 mwezi wa pili hivyo itakuwa ndiyo zawadi ya wapendanao kutoka kwangu mwaka huu 2009.
Siz Azizi anaongeza kuwa katika nyimbo hii ameibua kipaji cha mchezaji wa sinema Jaqulin aliyewahi kucheza filamu za Yelow Banana na The lost twins ambaye ameonyesha kipaji cha hali ya juu katika wimbo huo kitu ambacho kinanipa moyo kuendelea kumtumia katika nyimbo zijazo na kwamba kutokana na juhudi zake atakuwa mwanamuziki mzuri sana katika siku za usoni.

Siz Azizi aliwahi kutamba na wimbo wake wa kwanza ulinaoitwa (Kasoro) ambao alimshirikisha mwanamuziki Ray C. na hapo ndipo alipojulikana kwa mashabiki wa muziki wa Bongo Fleva na kujipatia sifa mialiko na mingi kutokana na wimbo huo, katika wimbo huo Siz Azizi alijulikana kwa jina la Sizy Q.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment