* Achanika kidevu, ang'oka meno mawili ukumbini
RAPAna mwimbaji nguli wa bendi ya muziki wa dansi ya African Stars 'Twanga
Pepeta International', Khalid Chuma 'Chokoraa', ameanza mwaka mpya wa 2009
vibaya, kwa kumwaga damu ukumbini.
Chokoraa alimwaga damu juzi usiku wakati Twanga Pepeta ilipokuwa ikitumbuiza
katika hafla ya kuukaribisha mwaka mpya 2009 kwenye ukumbi wa Triple A jijini
Arusha. Twanga ilitua Arusha baada ya mkesha wa mwaka mpya kupagawisha
mashabiki kwenye hoteli ya Safari Park jijini Nairobi, Kenya.
Akizungumza Dar es Salaam jana baada ya kurejea kutoka Arusha, Chokoraa
alisema aliumia vibaya na kupasuka chini ya kidevu, akang'oka meno mawili na pia
kupata maumivu sehemu za kifua baada ya kuteleza na kuanguka vibaya.
"Mwaka 2009 nimeuanza vibaya kwa kumwaga damu, Januari mosi majira ya saa 6
na ushei usiku kwenye shoo ya kufungua mwaka Arusha, katika mishemishe za
kupagawisha mashabiki nilikuwa nacheza shoo bize, nikatelekeza, nikafikia kifua na
kidevu, nikachanika na meno mawili kungo'oka," alisema Chokoraa.
Twanga Pepeta inayodhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Zain Tanzania,
imerejea nchini jana (Ijumaa) na leo inatarajia kuwachengua mashabiki kwa staili zake
mpya za 'Sugua Kisigino' ya Saulo John 'Ferguson', 'Nimeokota Kidude' ya
Chokoraa na Weka Selo, Kitumbua mbona wauza usiku, Obama, Wizi Mtupu na
Mambo Maregea za Msafiri Said 'Diouf'.
Chokoraa alisema Twanga Pepeta itaangusha moja moja kwa kuporomosha nyimbo
mpya zinazotarajiwa kuwemo kwenye albamu ya 10 ya bendi hiyo itakayozinduliwa
mwaka huu ikiwa ni pamoja na Sumu ya Mapenzi ambao ni utunzi wake, Shida
Darasa na Mtoto wa Mjini (Charles Gabriel 'Chaz Baba') na Nazi Haivunji Jiwe
(Thabit Abdul).
0 comments:
Post a Comment