Zain yazindua huduma ya simu Ghana!!


Ofisa Mtendaji Mkuu wa Zain Afrika, Bw. Chris Gabriel akiuza kadi ya simu kwa mteja wakati wa hafla ya Zain kuzindua huduma ya simu selula nchini Ghana, uzinduzi ulioambatana na kutoa huduma ya intaneti ya 3.5G jijini Accra, Ghana juzi.


· Yatambulisha mtandao wa intaneti wa 3.5G
· Yawekeza dola milioni 420 nchini Ghana
· Huduma ya ‘One Network’ yafikia nchi 17

Accra, Ghana – Desemba 15, 2008
ZAIN, kampuni ya simu inayoongoza kwa kutoa huduma katika nchi 22 Mashariki ya Kati na barani Afrika, imezindua huduma ya simu selula nchini Ghana, uzinduzi ulioambatana na kutoa huduma intaneti ya 3.5G kwa mara ya kwanza nje ya Afrika Kusini.
Mtandao wa Zain nchini Ghana utawawezesha wateja wake kupata huduma bora na ya haraka ya intaneti na kwa mara ya kwanza nchini Ghana watakuwa na uwezo wa kupokea simu zenye video ikiwa ni pamoja na kutuma picha za video, muziki na picha nyinginezo.
Huduma ya intaneti ya 3.5G ya Zain itawawezesha wananchi wa Ghana kuishi katika maisha mapya. Uzinduzi huo ulifanyika juzi katika mji mkuu wa Accra, na Zain imewekeza zaidi ya dola za Marekani milioni 420 kwa ajili ya kuimarisha huduma za mtandao huo nchini Ghana.
Kutokana na uzinduzi huo, Ghana imefanya idadi ya nchi zilizojiunga katika huduma ya ‘One Network’ kufikia 17. Huduma ya ‘One Network’ ya Zain isiyo na mipaka katika simu inatumiwa na zaidi ya watu nusu bilioni Mashariki ya Kati na barani Afrika – ambalo ni eneo kubwa kuliko Marekani.

Huduma ya One Network ya Zain ndiyo kitu ambacho kinapaswa kuangaliwa kwa hali ya juu kabisa katika mageuzi ya mfumo mpya wa kampuni. Kwa uzinduzi huo, wateja wa Ghana wanaweza kutumia huduma ya One Network wakisafiri katika nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Nigeria, Niger, Chad, Malawi, Gabon, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Congo Brazzaville, Burkina Faso na Sudan. Mashariki ya Kati, huduma ya One Network inapatikana katika nchi za Jordan, Bahrain, Iraq na Saudi Arabia.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Zain Group, Dkt. Saad Al Barrak alisema, “Tunaikaribisha Ghana katika familia ya Zain. Ghana ni muhimu kwa Zain na tumewekeza kwa nguvu zote ili kuleta teknolojia ya kisasa na huduma bora Magharibi mwa Afrika. Kutokana na mfumo wetu, tunawahakikishia watu wa Ghana watapata huduma bora ya mawasiliano duniani.”

Kutokana na Zain Ghana kujiunga katika huduma ya ‘One Network’, Bw. Chris Gabriel, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Zain Afrika, aliongeza kwamba: “Kutokana na maelfu ya watu wa Ghana kuvuka mipaka kila siku kwenda Burkina Faso na katika nchi nyingine zenye huduma ya ‘One Network’ ya Zain kama Nigeria na Niger, huduma ya One Network itaendelea kupanuka wigo wake na kuwawezesha wapendanao kupata mawasiliano kwa urahisi, na kuboresha maisha kwa jamii.”

Wateja wote wa Zain barani Afrika na Mashariki ya Kati waliounganishwa katika huduma ya prepaid na postpaid, wanatumia One Network na hivi sasa wanaweza kusafiri kwenda nchi 17 wakitumia simu zao bila kutozwa bei zaidi ya ile ya kawaida na bila kulipia gharama ili kupokea simu zinazoingia.

Wateja wa Zain pia wanaweza kuingiza pesa kwenye simu zao wakiwa nchi hizo bila kununua kadi kutoka nchi anayotoka na zaidi ya vituo 150,000 barani Afrika na Mashariki ya Kati vinatoa huduma kwa wateja wa Zain popote walipo.

“Wateja wanaweza kupiga na kupokea simu na kutuma ujumbe mfupi wa maneno kwa gharama za kawaida, kupokea bure simu zinazopigwa kutoka katika moja ya nchi 17 zilizounganishwa na huduma ya One Network. Huduma ya One Network kwa wateja wa prepaid inatolewa moja kwa moja katika nchi zote, na haihitaji mteja ajisajili wala kulipia ada," alisema Bw. Gabriel.

Zain inatambulika kwa kuongoza katika mageuzi ya teknolojia ya huduma ya mawasiliano ya kisasa kwa wateja inaowatumikia. Zain ilikuwa ya kwanza kuzindua huduma ya ‘One Network’ kwa zaidi ya watu milioni 100 nchini Kenya, Tanzania na Uganda mwaka 2006, na inaahidi kuendelea kutoa huduma bora za mawasiliano kwa wateja wa Zain

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment